Arsenal wameshinda rufaa mbele ya meza ya chama cha mpira wa miguu uingereza FA,kufuatia mamuzi ya kimakosa yaliyotolewa na mwamuzi Marriner.
Ambaye alitoa Penalti wakati wa
mchezo wa siku ya Jumamosi
baada ya Alex Oxlade-Chamberlain
kushika mpira, lakini Kieran
Gibbs alipewa kadi nyekundu na
kuondolewa kimakosa.
Oxlade-Chamberlain alionekana
akimwambia Refa kuwa yeye
ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo
uamuzi wa awali ndio ulikua wa
mwisho.