Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

CHANGAMKIENI SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI - KENYATTA

$
0
0
10004043_618718561545709_334195449_n
 RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akisalimiana na Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji mara baada ya  kufungua mkutano wa maalum wa Bunge la Afrika Mashariki jijini Arusha jana.

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amewataka nchi wanachama kuchangamkia nafasi katika soko la pamoja na ushuru wa pamoja wa forodha.

Akifungua mkutano wa maalum wa Bunge la Afrika Mashariki jijini Arusha, Rais Kenyatta amesema mawaziri wa Afrika Mashariki lazima waweke sheria na taratibu ili nchi wanachama zifaidike na malighafi za jumuiya.

Alisisitiza umuhimu wa jumuiya kuendelea na mazungumzo yenye tija kuhusu kushirikiana na jumuiya zingine za Afrika na hasa kusini mwa Afrika kama vile COMESA na SADC.
 Rais Kenyatta aliongeza kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki lazima ziunganishe nguvu kwa pamoja katika mapambano dhidi ya ujangili kwa sababu likiachwa linaweza kuua utalii katika nchi wanachama.

“kwa kipindi kifupi kati ya Januari na Oktoba mwaka jana zaidi ya tani kumi za pembe za ndovu zilikamatwa katika bandari ya Mombasa,” amesema.

Amesema pia kuna umuhimu wa kutafuta amani ya kudumu kwa nchi majirani na jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile Somalia na Sudan Kusini ili kuwapa nafasi wananchi kufanya mambo ya maendeleo.

“Vile vile ni muhimu kuondoa vizuizi vya biashara kwa nchi wanachama ili kufungua milango ya uwekezaji wa kiuchumi miongoni mwa wanachama (Non Trade Barriers).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>