Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI TEMEKE LEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajasiliamali-VICOBA mbalimbali katika mkutano uliofanyika mapema leo asubuhi  ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,katika Wilaya ya Temeke.Kinana aliwapongeza VICOBA hao kwa kuchapa kazi nzuri na kuwa waaminifu katika mazingira yao ya kufanya kazi.Aidha amewataka akina mama na vijana mbalimbali kutobweteka na badala yake wajitume kufanya kazi,katika suala zima la kujipatia maendeleo yao sambamba na kujikwamua na Umaskini.Ndugu Kinana amefanya ziara yake leo ya siku moja ndani ya Wilaya ya Temeke,ikiwa na lengo la Kuimarisha Uhai wa Chama hicho na kuhamaisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtemvu akielezea namna alivyoweza kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali katika kuunda VICOBA kwa ajili ya Maendeleo yao,katika Wilaya ya Temeke mapema leo wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokutana na VICOBA hao alipokuwa kwenye ziara yake ya siku moja wilayani humo.

Wana-VICOBA wakifuatilia mkutano 
 Meneja Mradi wa kiwanda cha kuzalisha gesi kilichopo kata ya Mtoni,Bwa.Richard Matari akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipotembelea mradi huo na kujionea hali halisi ya eneo hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi huo wa kuzalisha gesi na changamoto zake,Kiwanda hicho mpaka sasa hakifanyi kazi kutokanana kukumbwa na changamoto mbali mbali na kupelekea kusimama kutofanya kazi mpaka sasa. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Mkuu wa Mkoa,Mh.Meck Sadicky wakikagua mitambo ya kuzalisha gesi inayotokana na taka taka,kilicho Mtoni,wilayani Temeke.Kinana yuko ziarani wilayani humo kwa siku moja.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtevu akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa,Mh.Meck Sadicky nje ya ofisi za CCM,wilaya ya Temeke mapema leo asubuhi wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipoanza ziara yake wilayani humo.
 Katibu Mkuu wa CCM,akiwasili kwenye ofisi za CCM,wilaya ya Temeke mapema leo,ambapo alikutana na kamati ya siasa ya wilaya na kupewa taarifa kamili ya hali ya kisiasa ya wilaya hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipunga mkono kwa wananchi waliokuwa pembeni (hawaonekani pichani)  mapema leo asubuhi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar,Ramadhan Madabiba wakiwa ndani ya bajaji (hawaonekani),wakielekea kwenye mkutano mfupi wa kukutana na wajasiliamali-VICOBA,ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,wilayani Temeke.Kinana yupo wilayani humo kwa ziara ya siku moja.
 Baadhi ya akina mama mbalimbali waliojiunga kwenye VICOBA wakishangilia jambo,wakati wa mkutano mfupi uliowakutanisha na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,ambaye alizungumza nao na kuwatia moyo katika juhudi zao mbalimbali za kupambana na kujikwamua na lindi la umaskini.Kinana aliwaasa VICOBA hao kutobweteka na badala yake wafanye kazi kwa bidii na kujitegemea bila ya kusubiri ajira. 
 Mkutano ukiendelea
 Mwakilishi wa VICOBA wilaya ya Temeke,Mariam Temela akisoma hotuba yake fupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo asubuhi  katika Wilaya ya Temeke wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15 uliojumuisha VICOBA mbalimbali (hawapo pichani). 
 Mwakilishi wa VICOBA wilaya ya Temeke,Mariam Temela akikabidhi hotuba yake fupi aliyoisoma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo asubuhi  katika Wilaya ya Temeke wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15 uliojumuisha VICOBA mbalimbali. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>