KATIBU TAWALA WA MKOA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN AKIZUNGUMZA NA WAADISHI WA HABARI MCHAN WA LEO.
MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN AUGASTINE MGENDI AKIMUULIZA KATIBU TAWALA SWALI HUKU WAANDISHI WENGINE WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI.WAKATI WAKIPOKEA RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU TOKA KWA KATIBU TAWALA.
--
NA AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WARA BW. JOHN TUPPA UNATARAJIA KUAGWA KESHO NYUMBANI KWAKE KUANZIA SAA MOJA KAMILI ASUBUH MPAKA SAA TATU NA DK 20 MUSOMA MKOANI MARA NA BAADAE KUELEKA KANISA KUU LA ROMAN CATHOLIC PAROKIA YA MUSOMA KWAAJILI YA IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU KUANZIA SAA TANO ASUBUHI HADI SA 9:00 JIONI.
HAYO YAMESEMWA LEO NA KATIBU TAWALA WA MKOA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MCHAN WA LEO KATIKA UKUMBI MDOGO WA MIKUTANO.
OLE KUYAN AMESEMA KUWA MARA BAADA YA IBADA HIYO MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA MPAKA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AMBAPO UTAWASILI SAA KUMI NA NUSU ALASIRI KABLA YA KUSAFIRISHWA TENA HADI MJINI DODOMA AMBAPO UNATARAJI KUWASILI SAA KUMI NA MOJA JIONI NA KUHIFADHIWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA.
KWA KUWA ENZI ZA UHAI WAKE MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI MJINI DODOMA KAMA MKUU WA WILAYA WANANCHI MKOANI HUMO WATAPATA FURSA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU TAREHE 28 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI HADI SAA SITA MCHANA.
BW. OLE KUYAN AMEONGEZA KUWA BAADA YA WAKAZI WA DODOMA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SAA SITA MCHANA MWILI HUO UTASAFIRISHWA TENA HADI KIJIJINI KWAKE KILOSA AMBAPO UTAKABIDHIWA KWA FAMILIA YA MAREHEMU KWAAJILI YA MAOMBOLEZO SAA TISA ALASIRI.
MWILI WA MAREHEMU UTAFANYIWA IBADA IKIWA NI PAMOJA NA WANANCHI WA KILOSA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KWA MARA MWISHO KABLA YA KUPELEKWA KATIKA ENEO LA MAZISHI KWAA JILI YA KUUHIFADHI KATIKA NYUMBA YA MILELE SAA KUIMI NA MOJA JIONI.
MAREHEMU TUPA AMEFARIKI DUNIA JANA WILAYANI TARIME ALIPOKUWA KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI NA AMEACHA MKE NA WATOTO WATANO.
MAREHEMU ALIZALIWA JAN 1 1950.
MWISHOOOO…
----
TAARIFA TOKA TAASISI YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA YA MARA HOPE FOR LIFE (MHL) BIGAMBO JEJE,MUSOMA MARCH 26 2014,
TUPPA.
TAASISI YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA YA MARA HOPE FOR LIFE (MHL) IMEMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE:DK JAKAYA KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA MKUU WA MKOA WA MARA JOHN GABRIEL TUPPA ALIYEFARIKI DUNIA KWA GHAFLA AKIWA KATIKA KAZI ZA KUWATUMIKIA WANANCHI.
MKURUGENZI MKUU WA TAASISI HIYO YA WANAHABARI WA MKOA WA MARA BW. FAZEL JANJA AMEMUELEZEA MAREHEMU TUPPA KWAMBA WATANZANIA DAIMA WATAMKUMBUKA KWA MAMBO MENGI KATIKA KUWATUMIKIA WATANZANIA KATIKA NYADHIFA MBALIMBALI ALIZOZITUMIKIA KATIKA UADILIFU NA UAMINIFU MKUBWA.
BW. JANJA AMESEMA WAKATI WA UHAI WAKE HUSUSANI TANGU ALIPOTEULIWA NA RAIS KIKWETE KUTUMIKIA WADHIFA WA UKUU WA MKOA WA MARA MWAKA 2011, MAREHEMU ALIJITOLEA KWA HALI YAKE YOTE KUHAKIKISHA ANAWAHUDUMIA WANANCHI KATIKA KUWALETEA MAENDELEO KATIKA NYANJA KADHAA ZA ELIMU,MIUNDO MBINU,AFYA,MAJI NA KILIMO HUKU AKIMSIKILIZA KILA MWANANCHI NA KUTATUA KERO ZAO KWA KUTENDA HAKI BILA AINA YOYOTE ILE YA AMA UBAGUZI AU UPENDELEO.
AMETANABAISHA KWAMBA MAREHEMU TUPPA AMBAYE KIFO CHAKE NI PIGO KUBWA NA KIMEACHA PENGO LISILOWEZA KUZIBIKA KWA URAHISI, ENZI YA UHAI WAKE ALISHIRIKIANA NA VYAMA VYOTE VYA SIASA KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO HUKU AKIWAITA NA KUKAA NAO ILI KUJADILI NAMNA YA KUWEZA KUUENDELEZA MKOA KWA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA BILA KUWEKA TOFAUTI ZA VYAMA VYAO.
SALAMU HIZO ZA RAMBIRAMBI KWENDA KWA MHE:RAIS KIKWETE ZIMEONGEZA KUWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA WALIPATA USHIRIKIANO MKUWA NA WA KARIBU SANA TOKA KWA MAREHEMU TUPPA AMBAYE DAIMA ALIWAPENDA WANAHABARI NA KUWAPA KILA AINA YA USHIRIKIANO WALIOUTAKA TOKA OFISINI KWAKE NA KWAMBA KIFO CHAKE KIMEACHA PIA MAJONZI,SIMANZI NA HUZUNI ISIYO NA KIFANI KWA WANAHABARI WOTE.
MKURUGENZI HUYO MKUU WA TAASISI HIYO YA MHL BW. JANJA AMEWATAKA VIONGOZI KUIGA MFANO WA MAREHEMU TUPPA KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA KILA HALI NA KWA MOYO WA KUJITOLEA NA KUSISITIZA KUWA HATUA YA KUKUTWA NA UMAUTI AKIWA KAZINI NI USHUJAA,USHUPAVU NA UJASIRI MKUBWA AMBAO DAIMA JINA LAKE LITAANDIKWA KATIKA HISTORIA YA MASHUJAA WA HAPA NCHINI.
AIDHA AMEIOMBA FAMILIA YA MAREHEMU ALIYEFARIKI KUTOKANA NA SHINIKIZO LA DAMU AKIWA KIKAZI WILAYANI TARIME, KUWA NA UVUMILIVU,USTAHIMILIVU NA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WANACHOPITIA NA KUJIPA MOYO INGAWA KILA MMOJA ANATAMBUA KWAMBA MAREHEMU AMETANGULIA MBELE ZA HAKI HUKU FAMILIA HIYO IKIWA BADO INAMUHITAJI.