Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

WANAKIBINDU WASEMA :CHONDE CHONDE MH.RIDHIWANI UKIPATA UBUNGE ANZA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA KIBINDU

$
0
0
1Katibu  wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha kwa Msanja kata ya Kibindu katika jimbo la Chalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho, ambapo viongozi kadhaa wa Chama cha Mapinduzi  wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma wamewataka wananchi hao wa kata ya Kibindukumchagua mgombea ubunge wa CCM Bw. Ridhiwani Kikwete kwa kuwa anaweza kuwatatulia matatizo yao mbalimbali yanayowakabili  katika kata yao kwani Ridhiwani Kikwete ni msomi, mwanasheria na mtu aliyepewa dhamana na chama cha Mapinduzi chenye uongozi kuanzia shina mpaka ngazi ya kitaifa hivyo wanao uwezo wa kumpata mahali popote kwani anao udhamini wa kuaminika. hata hivyo tatizo kubwa la kata ya Kibindu ni miundo mbinu ya barabara na maji jambo ambalo wananchi hao wanaeleza kwamba ni muhimu mbunge wao anayekuja aanze nalo, Mbunge aliyepita Marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo aliugua muda mrefu jambo lililopelekea wananchi hao kukosa mwakilishi wao katika mambo mbalimbali ya maendeleo  jimboni humo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)2Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kwamsanja Kibindu leo.3Hii ndiyo hali halisi msafara wa viongozi hao ukielekea kijiji cha Kirumbi kwa ajili ya mkutano wa kampeni kijijini hapo.4Moja ya magari tuliyotumia likipita katika madimbwi makubwa.
5Gari hili likiwa limekwama na likisukumwa ili kunasua katika dimbwi la matope. 6Kwaya ikitumbuiza katika kijiji cha kwa Kirumbi.7Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kijiji cha Kwamsanja.8Wananchi wakiserebuka na muziki kjijini Kwakirumbi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.9Mtela Mwampamba kutoka UVCCM makao makuu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi.10Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwakirumbi.12Ukaguzi wa barabara ukifanyika kabla ya kupita.13Juhudi zikifanyika kunasua gari lililokwama.14Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita akipita na gari lake katika madimbwi.15Wananchi wakserebeka na muziki kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mjembe.16Baadhi ya morani wakifurahia jambo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Mjembe kata ya Kibindu.17Hapa mambo yamekaa sawa tunakunja vifaa na kunang’oa nanga.18Safari kuelekea kwenye magari

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>