Ndege ya Malaysia iliyopotea MH370.
Machi 8, mwaka huu dunia ilisikia vilio vingi kutoka Beijing, China na Kuala Lumpur, Malaysia. Ndugu, jamaa na marafiki walikusanyika viwanja vya ndege wakiwalilia ndugu zao waliopotea kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, Malaysia Airlines.Ilikuwa hivi; ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari namba Flight 370 kutoka Malaysia kwenda Beijing, ilipotea eneo la juu ya bahari katika Ghuba ya Thailand. Ukiondoa wafanyakazi na marubani, ilikuwa na abiria 239. Kati yao 159 ni raia wa China.
Ni takriban siku 20 sasa, ndege hiyo aina ya Boeing 777 (kubwa sana) haionekani. Hakuna mabaki yake! Tayari China, Marekani na mataifa mengine makubwa wamepeleka vifaa vyao kama satellite na radar kwa ajili ya kuitafuta ndege hiyo bila mafanikio (mpaka juzi).
IMEKWENDA WAPI?
Mwaka 2009, ndege kama hiyo ya Shirika la Ndege la Ufarasa nayo ilipotea duniani ambapo ilitafutwa bila mafaniko. Miaka miwili na nusu mbele, mabaki yake yalipatikana kwenye tope zito Kusini mwa Bahari ya Atlantiki.
Wataalam wengi duniani wa mambo ya usalama wa vyombo vya anga, wamekuwa wakizunguka angani na baharini ili kujua mahali ilipo ndege hiyo.
Kupotea kwa ‘dege’ hilo la Malaysia kumetishia kuvunja uhusiano wa China na Malaysia kwa tuhuma kwamba ulikuwa mpango.
ILITEKWA?
Taarifa za awali zilisema kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na duniani saa chache baada ya kuruka. Kuna wanaosema mawasiliano hayo yaliharibiwa makusudi kwani ndege hiyo ilitekwa. Lakini haingii akilini ilitekwa kwa sababu litafuata swali lingine ilitekwa ikapelekwa wapi hapa duniani?
MAKUNDI YA UGAIDI
Makundi ya kigaidi duniani kama Al qaeda hupenda kujitokeza wakati wa janga fulani na kudai wanahusika. Mbona katika hili hakuna kundi lililojitokeza?
Wengine wanadai labda watekaji waliibadilisha jina ikiwa angani na kwenda kutua sehemu nyingine! Maswali; imekwenda kutua uwanja gani? Kwa ratiba gani? Wale abiria 239 wako wapi?
Sawa. Hata kama ilitua mahali, kwa namna ambavyo teknolijia kwa sasa ni kubwa ingejulikana kwani kubadilisha jina kusingeifanya ndege hiyo isigundulike.
Hata hivyo, pamoja na mkanganyiko huo, kumekuwa na nadharia nyingi ya wapi ilipo ndege hiyo.
BLACK BOX
Kuna maelezo kuwa ndege zote aina ya Boeing 777 zina kisanduku maalum cha kutunzia kumbukumbu za mawasiliano ya marubani wa ndege na waongoza ndege walioko ardhini. Kinaitwa Black Box. Hata kama ndege ikilipuliwa au kupata ajali ya nchi kavu au majini, hakiwezi kuharibika.
Kifaa hicho kina uwezo wa kurusha mawimbi kuonesha kilipo kwa siku zisizopungua 30 baada ya ndege kuanguka.
Sasa wataalam wameshindwa kunasa mawimbi ya chombo hicho na hivyo kuwa na wasiwasi kwamba huenda kiliharibiwa kwa makusudi.
Sawa. Hata kama ndege hiyo ilianguka baharini, kwa nini mabaki yake hayakuelea juu ya maji?
Kulikuwa na tetesi kuwa kuna mabaki yalionekana zaidi ya kilometa 2,000 kutoka Australia, Kusini mwa Bahari ya Hindi lakini wataalam walipofika eneo hilo na vifaa vya uchunguzi, hawakuyaona.Aidha, kumekuwa na hofu kuwa huenda ndege hiyo imetoweka kabisa duniani. Lakini imekwenda wapi sasa?
ILIPIGWA KOMBORA?
Kuna waliosema ilipigwa kombora. Kama ndivyo, mbona kombora hilo halikuonekana kwenye vyombo vya uchunguzi vya kijeshi na vya usalama wa safari za anga? Ingepigwa kombora vingeonekana vipande vilivyosagika.
NJE YA NGUVU YA MVUTANO
Wengine wanaamini ndege hiyo ilipoteza uelekeo na kuruka umbali mrefu wa saa saba kama ilivyoelezwa kisha kutoka nje ya nguvu ya mvutano (gravitational force) hivyo kushindwa kurudi duniani.
Kama ndivyo, basi ndege hiyo itakuwa inaelea nje ya nguvu ya mvutano kwani kitu chochote kikishatoka kwenye Mfumo wa Jua (Solar System) hakiwezi kurudi tena.
MKONDO WA PEMBETATU
Kuna waliokwenda mbele zaidi wakidai kuwa huenda baada ya kupoteza uelekeo, ndege hiyo ilivutwa na Mkondo wa Pembetatu ‘Bermuda Triangle’ uliopo Kusini mwa Bahari ya Atlantiki (Kusini mwa Bara la Amerika) ambapo eneo hilo limekuwa likihusishwa na upotevu wa ndege za kijeshi na meli kubwa za mizigo.
Eneo hilo pia linahusishwa na viumbe wa ajabu waishio angani waitwao Aliens.
Baadhi ya wataalam wa sayansi wa kimataifa wanaiita sehemu hiyo makao makuu ya shetani kwa kuwa wenyewe hawajawahi kufika licha ya kwamba ni hapahapa duniani na wameweza kufika mwezini.
Kuhusu Aliens, wanasayansi wanakubali kuwa wapo, nao wamekuwa wakihusishwa na upotevu wa vitu na watu duniani. Inaaminika wana akili na teknolojia kubwa mno ambayo haipo duniani.
Baadhi ya wataalam wa anga wanasema viumbe hao wente shepu mbaya huenda wakahusika na kuitwaa ndege hiyo kuipeleka wanakojua wao.
NI FREEMASON?
Ukiachana na Aliens yapo madai ya ndege hiyo kuhusishwa na jamii yenye kuabudu mfumo wa imani ya Freemasons (Wajenzi Huru).
Wataalam wa masuala hay o wanaeleza kwamba ukiitazama hata nembo ya ndege hiyo iliyopo mkiani (kama bikari), ni moja kati ya alama za Freemason hivyo si ajabu wameamua kuchukua chao.
Wanakwenda mbali zaidi kwa kuvuta picha ya ramani katika eneo ilipopotelea ndege hiyo juu ambapo kwa chini ukiunganisha eneo moja na jingine inajitokeza taswira ya uso wa binadamu aliyekasirika.
Kwa wasioamini ishu za Aliens na Freemason, wanabaki na hitimisho moja tu kuwa ukweli ndege hiyo haikulipuka angani, haikuanguka baharini wala nchi kavu bali imetoweka duniani! Wataalam wanaendelea kuumiza vichwa. Ni tukio la kihistoria duniani!
Makala; imeandikwa juzi (Jumanne) wakati ndege hiyo haijapatikana.