STAA wa sinema za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema anapata wakati mgumu sana kufikiria kitu gani spesho atakachokifanya siku ya kumkumbuka aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba Aprili 7, mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’
Akipiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema siku hiyo ni siku ya majonzi makubwa kwake kwani anakumbuka siku ya kifo cha aliyekuwa mwandani wake na kila anachokifikiria kukifanya anaona hakikidhi.
“Naumiza kichwa, sijui hata nifanyeje ili kumuenzi vyema marehemu katika siku hiyo, napata wakati mgumu kwa kweli ila naamini siku siyo nyingi nitapata ufumbuzi,” alisema Lulu.