Mbunge wa Chadema John Wenje, aliyewahi kuwaita Wabunge wa CUF kuwa ni mashoga, leo ameuza kizaa zaa cha ajabu bunge la Katiba baada ya kuwaita Wajumbe 201 wasiokuwa wabunge kwenye bunge la Katiba Dodoma kuwa ni wala rushwa na kwamba wamekula rushwa kwa kupewa chakula, soda na bia na Mawaziri wa CCM. Mwenyekiti wa Bunge alipomtaka atoe ushahidi kama Sheria inavyosema, alishindwa kuutoa na kuendelea kuleta ubishi wa kitoto ndipo Mwenyekiti wa Bunge hilo Mh. Sitta alipomuamuru kwa mujibu wa Sheria za bunge hilo kuripoti mara moja kwa Kamati ya maadili ya bunge hilo na huko atatakiwa kuonyesha ushahidi wa tuhuma zake na suala hilo litarudishwa tena kwenye Bunge hilo kwa uamuzi.