Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Matuli kata ya Chalinze kwa ajili ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE).
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akishiriki kucheza muziki wakati mwimbaji Hafsa Kazinja alipokuwa akitumuiza katika kijiji cha Matuli kata ya Chalinze leo.
MNEC Martin Shigela akishiriki kucheza ngoma ya Kikwere wakati mkutano huo wa
kampeni. Msanii Dokii akishiriki kucheza ngoma iliyotumbuizwa na akina mama wa Kimasai katika mkutano huo wa kampeni.
Morani wa Kimasai wakishiriki kwa makini katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye kampeni.