Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MUUNGANO

$
0
0
IMG_0318Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif  Ali Iddi akizungumza na   waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu  masuala ya Muungano katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini Dodoma ljana.IMG_0322Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif  Ali Iddi akizungumza na  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  masuala ya Muungano katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)  mjini Dodomajana

Picha na Magreth  Kinabo – MAELEZO
Na  Magreth Kinabo- MAELEZO,DODOMA
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif  Ali Iddi amesema kwamba   Muungano wa Tanzania utakuwepo na  utaendelea kudumu, hivyo hakuna mtu atakayeweza kuuhujumu au kuuvunja kwa maslahi yake binafsi.
Aidha Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar amesema kauli iliyotolewa na Makamu wa Kwanza  wa Rais wa Zanzibar , Maalim Seif Sharrif Hamad hivi karibuni kuwa Wanzanzibari wote wanataka Muungano wa Mkataba si kauli ya kweli kwa kuwa hakuwahi kuzungumza na  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   wala wananchi, hivyo wananchi  wasitishike.
 Kauli hiyo imetolewa na Balozi Seif wakati   akizungumza na   waandishi wa habari kuhusu  masuala ya Muungano na mchakato wa Katiba Mpya  katika ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) mjini Dodoma jana.
“Wanzanzibari wengi wanauthamini Muungano tungependa kuuendeleza na kuihimarisha kwa maslahi ya pande zote za Muungano.
“ Katika mchakato huu,tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa kuonesha dhahiri ni zao za kutaka kuvuja Muungano kutokana na kauli zao . Kauli nyingi  zinatolewa zenye kuchonganisha wananchi  wa pande mbili za Mujungano,   alisema Balozi Seif.
 Alisema kwa mfano ,kauli za kusema Wazanzibari wote hawataki Muungano wanataka Mkataba “ Naomba kuuliza ni Wazanzibari gani hao wanaosemea  mbona sisi hapa pia ni Wazanzibari na hatuna msimamo huo wa mkataba? alihoji Balozi Seif.
 Akifafanua swali lililoulizwa na mwandishi wa  habari kuwa kauli aliyoitoa Maalim Sief kuwa ni ya Serikali,  Balozi Iddi alisema si kweli kuwa kauli hiyo ni  ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“ Maalim Seif kasema kama Katibu Mkuu wa Chama  cha Wananchi(CUF) wala si kwa niaba ya Serikali. Hakusema kama Makamu wa Pili wa Rais,” alisisitiza Balozi  Seif . Hivyo wananchi watambue kauli hiyo ni ya uongo na  hana uwezo wa kusema lolote.
 Aliwataka wananchi wa  Zanzibar  watambue kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   iko macho na yeyote atakayefanya fujo atashughulikiwa kikamilifu.
 Alisema Muungano una faida kwa  Wazanzibari kuliko Watanzania Bara katika umoja na kupanua wigo mpana wa matumizi ya ardhi,biashara na ajira.
 Akizungumzia kuhusu mchakato wa Katiba Mpya alisema unakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa uvumilivu miongoni wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bunge hilo kutawaliwa na hisia za kisiasa badala ya maslahi ya Taifa na kuna vikundi vya wachache wasiotaka mchakato huu uendelee kutokana na utashi wa kisiasa.
“ Vitendo vya uvunjifu wa amani kila siku ili Bunge liahirishwe kwa sababu tu za kibinafsi za baadhi ya wanasiasa  si jambo jema hasa kwa kuwa kodi ya Watanzania inapotea bila ya kufanya kazi iliyokusudiwa kuifanya na sisi waheshimiwa wajumbe, “ alisema huku akisisitiza kuwa  hali hiyo haitaweza kustahimiliwa.
Balozi Sief alisema wako katika Bunge hilo kwa kutetea maslahi ya Watanzania na sio mtu binafsi.
 Aliwataka viongozi hao kuwa mfano mwema wa matendo mazuri  mbel e ya jamii ya Watanzania na kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kustahimiliana na kuheshimiana ili lengo la Katiba  Mpya  liweze kutimia kwa maslahi ya taifa na Watanzania .
Akifafanua kuhusu makundi yaliyoundwa katika mchakato huo ambayo baadhi yao kuwa ni Tanzania Kwanza na  Ukawa kuwa  si rasmi bali yameundwa kwa utashi

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>