Kigogo wa kampuni ya kuchimba madini ya Afgem iliyopo Mererani mkoani Manyara, Abdallah Mwakaleja ‘Dullah’ anayedaiwa kupora mke wa mtu.
KIGOGO wa kampuni ya kuchimba madini ya Afgem iliyopo Mererani mkoani Manyara, Abdallah Mwakaleja ‘Dullah’ (38) anadaiwa kupora mke wa mtu, Violet Herman Masawe (29) huku ikisemekanaanatumia jeuri ya fedha kumnyanyasa mwenyemkeAkizungumza na gazeti hili, mume wa mwanamke huyo, Silvester Masawe mkazi wa Usa- River, Arumeru, Arusha alisema kuwa alifunga ndoa na Violet mwaka 2004 katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kalori, Usa River na kufanikiwa kupata mtoto wa kiume, Clinton Masawe (9). Mke wa mtu, Bi Violet Herman Masswe.
Mlalamikaji huyo alisema baada ya muda mkewe alibadilika tabia na kuanza dharau na kutomheshimu mumewe.Alisema aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kwamba mkewe huyo ana uhusiano ya kimapenzi nje ya ndoa. Hata hivyo, Masawe hakuweza kufahamu nani anayeingilia ndoa yake kwa kupindi hicho.
Siku ya ndoa kati ya Bi. violet Herman Massawe na Silvester Masawe mkazi wa Usa- River, Arumeru, Arusha.
Anaeleza: “Mgogoro ndani ya ndoa ulizidi kupamba moto. Watu, wakiwemo wazazi walisuluhisha ndoa yetu, amani ikarejea kwa muda ila sikuwa nikipatiwa unyumba kwa muda mrefu.”Alisema hali hiyo ilimfanya awe mnyonge huku mkewe akifanya atakavyo, ikiwemo kuondoka nyumbani na kurudi muda anaotaka akiwa na harufu ya pombe hali iliyomlazimu Masawe kuishi kama mkimbizi
ndani ya nyumba yake.
Mtoto wa miaka tisa ambaye Bw. Silvester Massawe amezaa na Bi. Violet .
Alieleza kuwa siku moja alisafiri kibiashara kwa muda mrefu na kumwacha mkewe akisimamia biashara nyingine ikiwemo nyumba ya kulala wageni, duka la jumla na rejareja.Hata hivyo, hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa kuwa mkewe hayupo nyumbani kitambo na baadhi ya bidhaa za dukani zimeyeyuka.
‘’Nilianza uchunguzi, ndipo nilipopata taarifa kuwa mke wangu anaishi na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Dr.Dril (Dullah),” alisema na kuongeza:
‘’Niliamua kufuatilia ila sikuelewa walipokuwa wanaishi, lakini nilibahatika kupata namba zake za simu na kumpigia. Alinijibu hanijui na nikitaka nikashitaki popote kwani anayo fedha na kwa vile mwanamke nilimtelekeza, nimemwona amependeza, namtaka, simpati ng’o.”
Alisema alikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Usa River juu ya upotevu wa familia yake ambayo ni mke na mtoto huku akimtaja anayemhisi.
Mwanaume huyo alisema polisi walimpigia simu Dullah na alifika kituoni. Alipoulizwa kuhusu kuishi na mke wa mtu wakati akijua ni kinyume cha sheria, alikiri na kusema alikuwa hajui kama mwanamke huyo ni mke wa mtu. Polisi walimuamuru kumrudisha mwanamke huyo kwa mumewe, lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Akizungumzia tuhuma hizo alipoongea na gazeti hili, Dullah alikiri kuishi na Violet na kujinasibu
kuwa mwanaume huyo hana hadhi ya kuishi na mwanamke mrembo kama huyo kwani akiwa kwake alimchakaza ila kwa sasa amenawiri.
‘’Huyo mwanaume alimtelekeza mke wake kwa muda mrefu, niliamua kuishi naye kama mke baada ya kumwona ana sifa zote,’’ alisema Dullah.
Alisisitiza kuwa, hana mpango wa kumwacha mwanamke huyo kwa vile ameshamnunulia gari aina ya Toyota Noah kwa ajili ya kutembelea tu. Kwa upande wake Violet, alisema hana mpango wowote wa kurudi kwa Masawe kwani kwa sasa ameanza maisha mapya na kilichobaki anafanya mpango wa kupata talaka ndani ya mwezi huu. - See more at: http://www.nyotanjematz.com/2014/03/ni-bonge-la-nomaa-mfanya-biashara-wa.html#sthash.6kv6Hae1.dpuf