Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

PUTIN AIONYA MAREKANI KUHUSU MCHEZO MCHAFU UKRAINE

$
0
0


Rais Vladimir Putin wa Russia ameionya Marekani juu ya kuwatisha kwa aina yoyote ile, raia wa Ukraine. Pitin ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu aliyofanywa na Rais Barack Obama wa Marekani na kumuonya asiyaunge mkono makundi yenye kufurutu ada nchini Ukraine yanayotoa vitisho kwa raia wasio na hatia wa nchi hiyo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika mazungumzo hayo ya simu yaliyodumu kwa muda wa saa moja, Obama na Putin walijadili kwa kina njia za kumaliza mgogoro wa Ukraine. Kwa mujibu wa White House, Obama amemwambia Rais Putin kuwa, ikiwa Moscow itarejesha nyuma askari wake kutoka katika mpaka wa Ukraine, basi Marekani nayo itakuwa tayari kutatua mgogoro wa nchi hiyo kupitia njia za kidiplomasia. 

Si vibaya kuashiria hapa kuwa, hadi sasa kuna wananchi wengi nchini Ukraine wenye uraia wa Russia. Hii ni katika hali ambayo Vitaly Ivanovich Churkin, mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, amesema kuwa, Moscow tayari imeshawasilisha mapendekezo yake kwa ajili ya kumaliza mgogoro wa Ukraine. Hayo yanatolewa katika hali ambayo nchi tofauti ikiwemo Afrika Kusini zimeendelea kutoa wito wa kutatuliwa mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>