Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MBWANA SAMATTA AIPELEKA TP MAZEMBE NANE BORA,SASA KILA KONA DRC JINA LAKE NDO HABARI YA MUJINI..

$
0
0




KLABU ya TP Mazembe imefuzu kutinga Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast 1-0 jioni hii Uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi.
Klabu hiyo ya tajiri Moisse Katumbi  imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia awali kufungwa 2-1 mjini Abidjan Jumapili iliyopita.

Ni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na mchezaji wa zamani wa Mbagala Market na klabu ya Simba , Mbwana Ally Samatta aliyefunga bao hilo pekee dakika za majeruhi za kipindi cha pili na kuirudisha timu hiyo ya DRC kwenye hatua ya makundi tangu mwaka 2012 waliposhiriki mara ya mwisho.
 
Ikumbukwe Samatta pia ndiye aliyefunga bao la Mazembe Abidjan ikifungwa 2-1 na maana yake yeye ndiye ameibeba kwa mabega yake timu hiyo hadi Nane Bora na sasa itasubiri kujua wapinzani wake watatu katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>