Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mhalinze wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Kibindu na kuhudhuriwa na wakazi wa kijiji hicho, akimuombea kura Ridhiwani Kikwete mgombea wa kupitia Chama cha Mapinduzi amemfananisha mgombea huyo na Jeki aina ya (Tanganyika Jack) na kusema atawakwamua wana Chalinze katika changamoto zinazowakabili katika maendeleo jimboni humo,Uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze unatarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu.(PICHA NA KUKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KIBINDU-CHALINZE)Kada wa Chama cha Mapinduzi kutoka UVCCM makao makuu Mtela Mwapamba akizungumza na wanakibindu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata hiyo leo.Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo wa kampeni
Msanii Puto akifanya vitu vyake katika mkutano huo.Wananchi wa kijiji cha Pera kata ya Kibindu wakiserebuka kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni kijijini hapo.Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kwamkonje kata ya Kibindu wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Mlau hayupo pichani.Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kwamkonje kata ya Kibindu wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mtela Mwapamba kutoka UVCCM makao makuu.Changamoto za ubovu wa Barabara kutokana na mvua leo pia ziliukabili msafara huo.Wakati mwingine ilibidi kuweka sawa barabara ili kuhakikisha msafara unapita na kuendelea na ratiba yake kama kawaida.Magari yakipita kwa kasi ili kuhakikisha hayanasi katika matope hayo.↧