Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Kigoma mjini bila kujali mvua,ambapo alisisitiza kuwa CCM itatekeleza kila walichoahidi.
Kila mtu alijikinga na mvua kwenye uwanja wa Mwanga Community Centre
Viti vikitumika kujikinga na mvua iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre wilaya ya Kigoma mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wa kwanza kulia),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Dk. Aman Walid Kaborou, Balozi Karume na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu wakati wa mkutano wa hadhara bila kujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa Peter Serukamba akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre na kuwaambia kuwa Kigoma imebadilika na bado anapigania wananchi hao wapate maji salama na ya kutosha.
Upinde wa Mvua unaonekanika kabla mvua kubwa haijanyesha kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo mkutano mkubwa wa CCM ulikuwa unafanyika.
Mjumbe wa NEC Balozi Ali Abeid Karume akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini na kuwaambia kuwa Muungano wa Serikali mbili ndio Muungano pekee utakaodumisha Umoja miongoni mwa wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo aliwaambia kuwa vyama vya upinzani vinaelekea kutoweka mapema kabla hata havijakomaa kidemokrasia.