Akiwa katika hali ya jazba na gadhabu, mhe. Tundu Lissu amejibu mapigo aliyopewa na mwasisi wa chama chake (CHADEMA) baada ya kauli zake chafu kwa baba wa taifa.
Tundu Lissu ambae pia ni mwanasheria wa CHADEMA, ameeleza kwamba yeye kama Mtanzania ana haki na uhuru kikatiba wa kutoa maoni yake. Hivyo atarajii mtu kama mzee Mtei aingilie uhuru wake huo.
Mhe Tundu Lissu pia aliongeza kwamba, yeye kama mjumbe wa bunge maalamu la katiba, ana uhuru wa kikanuni wa kuongea jambo lolote ila tu lisivunje sheria za nchi. Hivyo haoni kama kauli yake kwa baba wa taifa imevunja kipengere chochote cha sheria.
Aidha, Tundu Lissu pia ameomba Watanzania waache unafiki kwa kujifanya wamechukizwa na kauli zake kwa Nyerere, wakati Nyerere ndio chanzo cha migogoro yote hii tuliyonayo ikiwemo suala la muungano na serikali zake.
Source - JF