MSANII wa maigizo na filamu nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ ameeleza kuwa, kwa furaha aliyonayo baada ya kupata safari ya kwenda Uturuki imemfanya ajisikie kufa kwani ni bahati ambayo hakuitarajia.
Mzee Majuto amepata shavu akiongozana na wasanii wengine wawili, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Steven Jacob ‘JB’ ikiwa ni mualiko wa Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na mkewe Yasim kwa udhamini wa Princes Casino. Akizungumzia safari hiyo, Mzee Majuto alisema:
“Kwa kweli furaha niliyonayo najisikia kufakufa tu, ngoja ninyamaze kwa sababu bila hii safari huenda ningedoda hapa Tanzania mpaka nakufa, nashukuru sana watu wa Princes.”
Mastaa wengine waliotakiwa kuwemo kwenye msafara huo ni pamoja na Aunt Ezekiel na Wema Sepetu lakini kutokana na kubanwa na majukumu mengine, wameshindwa kuondoka.