Kwa kipindi hiki kijana Amos, ambaye anatoka Kata ya Mryaza, amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, lakini matarajio ya kupona kwa tiba za hapa nchini hayapo hivyo njia pekee iliyobaki ni kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Kijana Amos Ng’arare Sasi (21) mkazi wa kijiji cha Kizaru wilayani Musoma Vijijni amepoteza mwelekeo wa maisha baada ya ndoto yake ya kusoma hadi chuo kikuu kuishia njiani kutokana na matatizo ya ugomjwa wa ajabu ambao umemtesa kwa kipindi cha miaka 17.
Kwa kipindi hiki kijana Amos, ambaye anatoka Kata ya Mryaza, amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, lakini matarajio ya kupona kwa tiba za hapa nchini hayapo hivyo njia pekee iliyobaki ni kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Katika mahojiano na Mwananchi wiki iliyopita akiwa Wodi Namba 21, Sewahaji, Amos alionekana mwenye mawazo kupita kiasi.
“Ndoto yangu ya elimu itakuwa imeishia hapa. Sitegemei kurudi tena. Wenzangu niliokuwa nikisoma nao darasa moja, kwa sasa wapo kidato cha nne. Nilizaliwa nikiwa sina tatizo la aina yoyote kiafya na nililelewa na wazazi wote wawili. Kwa kweli kwa malezi niliyoyapata, sikuwahi kujiona tofauti,” anasema.
“Nikiwa na miaka minne baba alifariki dunia, nikabaki na mama ambaye alitulea mimi na kaka yangu kwa furaha akijishughulisha na kilimo cha jembe la mkono,” anasema Sasi.SOMA ZAIDI >>>>>>>>