Bwana Gasto Edward na mkewe ambaye anadaiwa kumkata nyeti zake.
Gasto Edward (32) amemkata mkewe Mwelu Raymond sehemu zake za siri, Risasi Jumamosi lina simulizi hii ya kusikitisha. Tukio hilo lilitanguliwa na kumpiga mkewe huyo na kipande cha nondo kichwani hali iliyosababisha apoteze fahamu papo hapo na kutekeleza azma yake.Imeelezwa kuwa, tukio hilo lenye sura ya majonzi, lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Jumatano ya wiki hii, huko King’azi, Kwembe – Mbezi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
KISA CHA YOTE
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa, chanzo cha unyama huo ni wivu wa kimapenzi ulioingilia ndoa hiyo, ambapo Gasto alimtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayeishi Temeke aliyejulikana kwa jina la Mgogo.
Chanzo chetu cha kuaminika, kwa sharti la kutotajwa gazetini kilisema: “Mwelu na Gasto wametoka mbali, wameishi kwa muda mrefu na wamebarikiwa watoto wawili, sema siku za hivi karibuni, Gasto alianza kumtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa.Soma zaidi hapa >>>>>>>>>>>>>