MSANII wa Bongo Fleva,Vanessa Mdee(v – money) amefunguka kuwa yeye alikua miongoni mwa majaji waliopiga kura kwa ajili ya wasanii waliotajwa kwenye categories za tuzo za BET Awards 2014.
Majaji hao wanakua 500 kutoka barani Africa, UK na Marekani ambako tuzo hizo zinafanyika kila mwaka tangu mwaka 2001, na mwaka huu msanii Diamond Platnumz ataiwakilisha Tanzania kwa mara ya kwanza Vanessa amefunguka mchakato ulivyokuwa na kura yake ilienda kwa nani.