HUYU DIAMOND HUYU....DAAAH! ETI WANASEMA NANII MKALI ZAIDI YAKO, ACHANA NAO, HUYO NAMFANANISHA NA ARSENAL (KABLA YA KOMBE)
Hebu niambie, unajisikia kumchukia mtu halafu anazidi kupata mafanikio? Moyo unauma au roho inakusuta?
Kwa kipindi kirefu sana tulikuwa tunahitaji msanii yeyote kutoka Tanzania aje atuwakilishe kimataifa, alipoanza kuibuka AY, tulifurahi sana kwa kuona kwamba sasa hivi tunakwenda kutangazwa Kimataifa.
Ay akajitahidi sana kadri alivyoweza lakini tukapuuzia, yaani jitihada zake zote, watanzania tukashindwa kuzikubali sana japokuwa kila siku hilo ndilo lilikuwa lengo lake, Tanzania ifike sehemu ambayo nayo itapata heshima.
Baada ya AY, akaja Lady Jay Dee, naye kama alivyokuwa AY, akajitahidi sana, akaachia ngoma na wasouth, yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa nchi yetu, tukamsifia sana Lady Jaydee, yeah! Ukweli ni kwamba alifanya vizuri sana.
Maisha hayo yamekuwa kama tamthilia fulani inayoendelea, baada ya AY kutoa season One yenye episode za kumwaga, Jaydee akaja na Season Two, naye akatuwekea episodes za kumwaga.
Leo hii, Diamond amekuja na muendelezo wa tamthilia yetu, season Three yenye episodes za kumwaga ambapo mpaka sasa hivi tumeangalia episodes tatu tu.
Alikuwa masikini fulani tu kule Tandale Uzuri, nyumba aliyokuwa akiishi sijui na bibi yake ni ya hadhi ya chini sana, hata yetu nzuri. Kama unavyopitia katika maisha, jamaa naye alipitia hivyohivyo tena inawezekana yeye akawa zaidi.
Leo hii, amepiga hatua mbele, amefika mbali ambapo hata AY na Jaydee hawakuweza kufika, tunakaa kumdiss kila wakati. Swali linakuja, kwa nini tunamdiss na wakati anaendelea kufanya vizuri?
Naweza kujibu kidogoooo, washikaji wanasema kwamba jamaa anaringa, sawa, hayo ni maisha ya mtu binafsi, mbona wakina Justin Bieber wanaringa lakini bado tu watu wanawafagilia? Diamond kawa nani bwana?
Wakati alipowasaidia watoto kusoma katika shule ya International, watu wenye chuki hawakusema bali wao wanaangalia leo kafanya nini baya ili waongee.
Mtu anapofanya vizuri, daima apewe sifa na anapofanya vibaya, basi asifiwe. Kila siku kilio changu kilekile, watu wa Uswahilini ndiyo wenye chuki binafsi, walitamani Diamond awe pale alipokuwa kama zamani.
Wengine wamezua mijadala, wanauliza kati ya Diamond na Ali Kiba nani mkali? Wengi wanasema Ali Kiba, sawa, huo ni mtazamo.
Huyo Ali Kiba yupo wapi? Uzuri wa timu ni makombe. Lilikuwa ni jambo lisilokubalika kuiita Arsenal timu bora na wakati haina kombe kwa muda mrefu mpaka ilipopata kombe.
Ili tujue timu yetu nzuri, kombe kwanza, si sawa jamani? Sasa huyo aliyekuwa mkali kuliko Diamond kapata tuzo gani? Eti wanasema promo, kitu kizuri siku zote hujiuza hata kama hakuna promo, jua hilo.
Acheni mapungufu aliyokuwa nayo, kila binadamu anayo ila linapotokea suala la kazi, hebu tuangalie, anafanyaje kazi, je ni nzuri au mbaya.
Leo hii nilipokuwa napitia page ya BET Award nilishangaa sana baada ya kuona msela akiendelea kuwaburuza vibaya wakina Davido, Mafikizolo, Savage na wengine. Mpaka sasa hivi, ana asilimia 78 ya kura za BET huku wa pilisi akiwa Davido mwenye kura asilimia 29, bado mpaka hapo mnamuwekea majungu kwamba jamaa anabebwa, hebu niambieni, anabebwa na nani.
Hebu pitia hapo kwenye page ya BET Awards. Jamaa anawapelekesha wagombea wengine kwa kupata LIKES nyingi ambazo zinaonyesha ni kwa jinsi gani anapendwa.
Kumbuka kwamba 80% ya watu walioLIKE page hiyo ni nje ya Africa, mshikaji wamemjuaje kama si kujitangaza?
Kwa watu wanaogombania kuchukua tuzo mbalimbali, Diamond kawazidi Future (Mwanamuziki kutoka Marekani), Mayweather (Mwanamasumbwi), Eve (Mwanamuziki), Kelvin Durant (Mcheza Kikapu), Drake (Mwanamuziki), Davido (Mwanamuziki), Beyonce (Mwanamuziki) na wengine wengi, yaani aliyekuwa juu zaidi yake ni mmoja tu, huyo ni Chriss Brown.
Kwa kawaida LIKE hazitoi tuzo lakini zinaonyesha ni kwa jinsi gani wadau wanakukubali. Tuacheni majungu, hebu fanya kumsapoti huyu mshikaji kimataifa kwa sababu hata ukisema umsapoti huyo aliyekuwa mkali zaidi yake bado haisaidii kwa sababu yeye ni kama ARSENAL, miaka mingi bila kombe.Huyuhuyu tuliye naye ambaye anatungaza sana hebu tumsapoti kwa sababu hii ndiyo nafasi pekee ya kufanya hivyo.
Tuacheni fitina, kama jamaa anafanya vizuri tumkubalini tu kwani hata tukimkataa, wazungu washamkubali.

Kama yeye ni mkali, juzi kati alitoa nyimbo kali, mbona hazikuhit? Leo hii, sisi watanzania hatumkubali Diamond, cha kushangaza, nchi za wenzetu kama Nigeria, Ghana na nyinginezo wameonekana kumkubali sana jamaa, au ndo nabii hakubaliki kwao?
Kama kweli jamaa promo ndo zinamuweka juu na kutangazwa sana, mbona mchizi anajitahidi hata kufanya ngoma na washikaji wa nje? Hebu vuta picha endapo Diamond angepata nafasi ya kuimba wimbo ule na R Kelly, kweli asingeweza hata kutoa naye nyinmbo kizushi? au hata kama angeshindwa, unafikiri angekuwa hapo?
Ninachopenda kutoka kwa msela ni kwamba kaamua kuutangaza muziki, nyie semeni, yeye hata habari. Leo anatumia mamilioni kurekodi video, anapata faida gani kupitia hiyo video zaidi ya kujitangaza zaidi?