Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.
kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao asubuhi ya Juni tano mwaka huku,akiwa uchi wa mnyama,ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tangu kutoweka kwa kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio huku wakihusisha tukio hilo limefanywa kwa imani za kishirikina.Soma zaidi hapa >>>>>>