Mapenzi ya Nuhu Mziwanda na Shilole yanazidi kupiga hatua na kuwa surprise kwenye story za mahusiano ya mastaa wa bongo.
Nuh Mziwanda ameamua kuuonesha upendo wake kwa vitendo zaidi kwa kujichora tattoo ya jina la Shilole ‘Shi Shi Baby’ na kwa msisitizo Tattoo hiyo haifutiki.
“Coz nampenda mke wangu nimeamua kuchora jina lake! Ila imeuma kuliko tattoo iliyopita! Siju kwa nn?” Ameandika Nuh Mziwanda.
Nae Shilole alipost picha hiyo na kuandika, “Thankx my lv 4 dis! Umeonesha love ya ukweli.”
Nuh ataishi maisha yake yote akiwa na tattoo hiyo.Tunatumaini ataishi maisha yake yote akiwa na Shilole pia.