“Sijawahi kuona mwanamke mzuri na mwenye imani kama mama Komba ( Salome ) jamani, unajua kulea watoto ambao mama zao wapo duniani ni kazi sana,”alisema Komba katika kipindi cha mkasi kinachorushwa na East African Television
Mheshimiwa Komba alisema ana watoto tisa wakiwemo wa ndani ya ndoa na nje ya ndoa na wote wamelelewa na mke wake Salome na ndio maana anampenda na kumjali kila siku za maisha yake kwani anastahili kuitwa mwanamke haswa…..
John Komba aliyasema hayo siku chache baada ya kuonekana picha zake mbaya za kimahaba alizopiga akiwa na msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake…..
“Sioni ajabu kuzushiwa mambo ambayo sijayafanya kwani wanamuziki, wanasiasa na hata viongozi mbalimbali wanakutana na mambo ya kuzushiwa kwa kuwa wanajua wakifanya hivyo watawaangusha kutokana na vyeo vyao lakini bado tupo bana,” alisema Komba huku akicheka.
Komba aliendelea kuzungumza kuwa mwaka 2015 utakuwa mwisho wake kuimba na anakusudia kuwarithisha vijana wapya….
Mheshimiwa Komba alihitimisha kwa kusema kuwa katika maisha yake hafikirii suala la kufa kwani kifo kipo tu hata ukifikiria na kukaa kuwaza jambo hilo ni kujitafutia mkosi tu katika maisha yako.