Makundi mawili hasim ya wasanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja yajulikanayo kama 'Wema Team' na 'Kajala Team' yanatarajiwa kuvunjwa kwani ndio yameonekana kuchochea bifu la wawili hao ambalo limekuwa likionekana kuisha na kuibuka tena....
Akizungumza na mwanahabari wetu, Kajala amesema kuwa tatizo lao limekuwa likichochewa na makundi hayo hasa wanapotangaza kusamaheana na kuzika tofauti zao makundi hayo huibuka na kuanza kutukanana, kitu ambacho huzusha tena hasira zao....
"Siyo siri, tatizo letu linachangiwa na hizi team ambazo zipo kwa ajili ya kuongeza matatizo.Tunafikiria kuyavunja kwani kwa sasa yameonekana kutokuwa na faida zaidi ya kuzidisha hasira ambazo tumekuwa tukizizika kila tunapotangaza kusameheana," alisema Kajala.
Msanii huyo alisema hawaoni haja ya kuwa na makundi ambayo hayawatakii mema kwani katika maisha kukosana kupo lakini pia kusameheana ndo jambo la busara kwani hakuna aliyemkamilifu hapa duniani.