Mwanamke mmoja ameamua kujitokeza hadharani na kusema kuwa katika maisha yake tayari amekwishatembea na wanaume elfu 10 asilimia 90 wakiwa wameoa katika harakati zake za kujitafutia kipato.Gwyneth Montenegro alikulia nchini Australia katika shule binafsi kabla ya kwenda kuwa mmoja wa wasichana makahaba wanaolipwa pesa nyingi zaidi akipata zaidi ya dola 2,000 kwa usiku mmoja kutoka kwa wateja wake.
Anafafanua zaidi sababu za kujiingiza kwenye biashara hiyo moja ikiwa ni kutokujiamini na kutaniwa sana alipokuwa shule kutokana na kuwa na aibu sana hivyo kupelekea wanafunzi wenzie kumchokoza.
Wakati wengi wa marafiki zake waliishia kuwa madaktari na wengine wanasheria, Gwyneth aliingia katika biashara hiyo na kufanikiwa kulala na wanaume 10,091 na kuweka taarifa za kumbukumbu ya kila mmoja wao.