Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amekana kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kuwa miongoni mwa watu ambao wanamiliki mabasi ya UDA.
Ridhiwani amekana hayo leo kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa huo.
Ridhiwani alisema kuwa anasikitishwa na kuumizwa na watu wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kuwa yamekuwa yakiathiri vijana kwa namna mbalimbali na pia alikana kuhusika na biashara ya mafuta na gesi pamoja na kumiliki kampuni ya mabasi inayomiliki mabasi ya UDA.