Ndugu wa marehemu akiuandaa mwili kwa ajili ya kuagwa
SAKATA la wafanyakazi wa ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika sura ya kipekee, safari hii mabosi wamegeukwa ambapo mmoja amedaiwa kuuawa na hausigeli wake aliyetajwa kwa jina la Valentina Karenge (17).
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi huyo wa ndani mkoani Singida kudaiwa kumuuua tajiri yake kwa kumchoma kisu sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyaswa naye. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake lilijiri saa 10 alfajiri Juni 29, mwaka huu eneo la Sabasaba, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida. Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Pendo Justine Kiula (24) ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.