Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA MAENEO KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA VIJANA

$
0
0
IMG_5027
Mmoja wa wanakikundi wa Kikundi cha Vijana cha Maamuzi, Bw. Juma Ismail Hassan (aliyevaa tshirt ya blue) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kikundi hicho na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) alipotembelea kikundi hicho mwishoni mwa wiki Kilwa Kivinje, Mkoni Lindi.Katibu Mkuu aliktembelea kikundi hicho ambacho kiko kwenye hatua za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya ili kukihamasisha kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo na badala yake wajikite katika shughuli za uzalishaji.
IMG_5042
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Maamuzi pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Kilwa. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi, anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bw. Charles Mwaitege na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilwa, Bw. Simon Manjurungu na wa kwanza kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Lindi, Bibi Makalaghe Shekalaghe Nkinda.

IMG_5048
Katibu wa Kikundi cha Sayari, Bibi. Mwanaisha Ali akikabidhi Risala ya Kikundi hicho kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga mwishoni mwa wiki alipotembelea kikundi hicho kwa ajili ya kukagua maendeleo ya shughuli za vikundi vya Vijana Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi.
IMG_5055
Mwenyekiti wa Kikundi cha Sayari, Bw. Ramadhan Sungura akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati alipokutana na kikundi hicho kwa ajili ya kukagua maendelo ya shughuli za kikundi hicho mwishoni mwa wiki.
…………………………………………………………
(Na Concilia Niyibitanga)
Halmashauri zote nchini zinawajibika kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijana pamoja na kuwatengea vijana asilimia 5 ya mapato ya halmashauri husika kwa ajili ya kuwezesha shughuli hizo.
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga wakati akikagua maendeleo ya vijana Wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
Amesema kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa na kwa maana hiyo wanatakiwa waongozwe na wawezeshwe ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa lengo la kujikwamua katika umaskini.
Vijana wanatakiwa kuhamasishwa kuunda na kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuunda SACCOS za vijana ili waweze kupatiwa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kuongeza mitaji na kupanua uzalishaji. Amesema Bibi Nkinga.
Akiongea na Kikundi cha Vijana cha Maamuzi kilichopo Kilwa Kivinje ambacho kina wanachama 21 ambao hapo awali wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na sasa kuamua kupunguza matumizi ya madawa hayo, aliwataka kuendelea kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kwani madawa hayo yanaathiri afya zao na kupunguza uwezo wa uzalishaji.
Aidha, alikitaka kikundi hicho kuendelea kuwahamasisha vijana wenzao walioathirika na madawa hayo kujiunga katika kikundi hicho ikizingatiwa kuwa Wilaya ya Kilwa ina Vijana zaidi ya 100 walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.
Aliwataka kuendelea kushiriki katika shughuli za kujitolea wanaozifanya sasa za usafi wa mazingira na wasikate tamaa wasonge mbele kwa kuwa familia zao na jamii nzima inawategemea wao kama nguvu kazi ya taifa.
Wakati huo huo, akiongea na kikundi cha vijana cha Sayari chenye wanachama 22 kinachojihusisha na biashara ya uuzaji chakula cha mifugo aliwataka kuendelea kuwa wabunifu na kuanzisha miradi mingi zaidi ya kuwaingizia kipato na kutunisha mfuko wao.
Pia aliwataka kuhakikisha kuwa wanasajili kikundi chao ili kiweze kutambulika kisheria na pia wajiunge katika SACCOS ya vijana ili iwe rahisi kupatiwa mikopo ya kuendeleza shughuli zao za uzalishaji mali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>