MMTANGAZAJI wa Redio EFM aliyewahi kuanguka kimahaba na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amewafungukia wanaomshangaa kuhusu kufunga mwezi wa Ramadhani na kuwataka watu hao wasimshangae kuhusiana na jambo hilo.
Akifafanua ishu hiyo mbele ya mwandishi wetu, staa huyo alisema kuwa amezaliwa katika familia yenye dini mbili japokuwa yeye ni Mkristo, lakini hufunga Ramadhani na Kwaresma sambamba na kusheherekea sikukuu zote kwa kuwa familia yao huamini Mungu ni mmoja.