Mwenyekiti wa Yanga amemaliza kikao na waandishi wa habari kuhusu kufungwa jana na Simba, amesema lawama zote zielekezwe kwake na sio mwingine yoyote na kwamba Yanga haijaamua hatma ya Kocha wa sasa wa timu iwapo aendelee au asimamishwe ila vikao vya Viongozi wa timu hiyo vinaendelea sasa hivi kabla ya kutoa uamuzi wao rasmi.