MNAMO TAREHE 12.01.2014 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LEMA NA KATA YA NGANA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. BICCO S/O MWAKIBIBI, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LEMA ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE NA FIMBO. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU NA MWENZAKE KUVUNJA KIBANDA CHA BIASHARA NA KUIBA, MWENZAKE ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 12.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:30HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. ADAMU S/O SILUMBE, MIAKA 27, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KAPELE ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALICHOMWA KISU MGONGONI TAREHE 10.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS NA MDOGO WAKE AITWAE BONNY S/O SILUMBE KATIKA KIJIJI CHA KAPELE, KATA YA KAPELE, TARAFA YA NDALAMBO. CHANZO NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MAREHEMU KUMTANGAZA MTUHUMIWA HAPO KIJIJINI KUWA ALIMTOROSHA MKE WA MTU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUSHUTUMIANA NA BADALA YAKE WATATUE MIGOGORO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.