Mrembo wa Tanzania aliyewahi kulivaa taji la Miss Tanzania 2004, Faraja Kotta Nyalandu, ameendelea kujikita katika miradi ya kuwasaidia wanafunzi ili kuongeza ubora kwenye elimu ya Tanzania.
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu azindue tovuti yake maalum kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa O-Level kwa ajili ya kukabilia na changamoto za masomo yao, hivi karibuni mrembo huyo ambaye ni mwanzilishi wa Shule Direct anatarajia kutoa kitabu maalum chenye mbinu Kumi zitakazomsaidia mwanafunzi kukabiliana na masomo yake.
Kupitia Instagram, Faraja Kotta ameandika kuwa tayari kitabu hicho kimekamilika na akaambatanisha picha vitabu kadhaa kikiwemo kitabu hicho kinachoitwa 'Mbinu Kumi za Kumudu Masomo Yako'.
“#Unaweza #SneakPeek. Mbinu Kumi za Kumudu Masomo Yako. Kitabu kipya kutoka kwangu kwaajili ya wanafunzi. Jenga uwezo. #KikoTayari #ItsReady.” Faraja ameandika.
Mrembo huyo amepewa sapoti na Miss Universe Tanzania 2007, Flavian Matata ambaye amenukuu maneno yake na kuandika, “Proud of You Faraja, this is amazing.”