Wasanii; Diamond Platnum na Wema Sepetu wametua rasmi mikononi mwa mdau wa sanaa nchini, Ruge Mutahaba kwa ajili ya kuandaliwa taratibu za kufanya kazi nyingi zinazohusu muziki na filamu.
Nyota hao wawili ambao wamekuwa na maisha mithili ya maigizo, kutokana na kuvurugana kila wakati katika uhusiano wao, inadaiwa kuwa wameafiki kufanya kazi za filamu chini ya Mutahaba.
Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi, Utafiti na Uzalishaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, amekiri kuingia makubaliano na wasanii hao, ila akasema ni mapema sana kutangaza juu ya kazi alizopanga kufanya na wakali hao.
"Ndio nimeingia makubaliano ya kazi na wasanii hao, Wema na Diamond ila yote yatasemwa siku chache zijazo, hivyo naomba wadau wa wasanii hao wasubirie vitu vingi kutoka kwao," amesema Mutahaba
Dar es Salaam, Tanzania.Nyota hao wawili ambao wamekuwa na maisha mithili ya maigizo, kutokana na kuvurugana kila wakati katika uhusiano wao, inadaiwa kuwa wameafiki kufanya kazi za filamu chini ya Mutahaba.