Dar es Salaam. Kocha Luc Eymael amemponda kocha mpya wa Yanga, Mdachi Hans Van der Pluijm akisema hawezi kuipa timu hiyo mafanikio kwani hajafanya jambo lolote la maana katika soka ukilinganisha na yeye.
Eymael ambaye ni raia wa Ubelgiji alikuwa miongoni mwa zaidi ya makocha 50 waliotuma maombi wakitaka wapewe kazi ya kuinoa Yanga, lakini alitoswa baada ya uongozi wa klabu hiyo kumpa fursa hiyo Pluijm. Akizungumza na gazeti hili, Eymael alisema, uongozi wa Yanga umefanya uamuzi usio sahihi kumwacha, kwani anaamini alistahili kupewa kazi hiyo kutokana na kuwa na wasifu mzuri kuliko wa Pluijm.
“Kitu ambacho nina uhakika nacho, wasifu wangu na wa kwake haufanani hata kidogo, lakini ni uamuzi wao na maisha yanaendelea. “Naamini kadri muda unavyokwenda ukweli utafahamika, tatizo Afrika makocha hawapimwi kwa uwezo wala wasifu, wanaangaliwa mambo mengine ambayo hayana msingi,” alisema Eymael
Aliongeza: “Ni kama nilivyokuambia awali kuna wakati nilifanya mazungumzo na AFC Leopard, lakini dakika za mwisho wakampa kazi Tom Olaba. Aprili wakaniita wakati timu ipo katika nafasi ya 13 kati ya timu 16, nadhani sipewi heshima ninayostahili.”
Alisema, anavyofahamu Pluijm anarekodi za kufukuzwa kila wakati hivyo hatua ya uongozi wa Yanga kumpa kazi ya kuifundisha timu yao imemfanya aamini hawana nia ya dhati ya kusaka mafanikio.