Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

KUFURU!!PARTY YA VIJANA WA KILEO NI MAJANGAZ POMBE ILIVYOWACHANGANYA


WATANZANIA WAOMBWA KUTEMBELEA BANDA LA ACCESS BENKI LILILOPO SABASABA ILI WAJIPATIE MKOPO WA CHAP CHAP

$
0
0

Wafanyakazi wa Access Benki, Frida Moshi akielezea machache wakati akihojiwa na Channel 10 kuelezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Access Benki, Catherine Gyumi akielezea machache wakati akihojiwa na Channel 10 kuelezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Bi. Gyumi alisema kwa sasa benki yao imeanzisha huduma ya 'ACCESSBANK WAKALA' wanaomrahisishia mteja kutoa na kuweka pesa akiwa mtaani kwake hakuna haja ya kwenda benki. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON  BLOG.
Afisa Mikopo wa Access Benki, Mwajabu Mhone akielezea machache wakati akihojiwa na Channel 10 kuelezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ambapo Mhone aliwaomba watanzania kufika bandani kwao ili kujipatia mikopo ya chap chap inayotolewa kwa wajasiliamali wadogo na wakubwa.
Afisa Masoko Msaidizi wa Access Benki, Humphrey Masudi akiwaomba watanzania wateja wa benki hiyo kuitumia kikamilifu huduma ya 'RAHISI' inayomsaidia mteja kuweza kutoa na kuweka pesa popote alipo kupitia simu yake ya mkononi... piga *150*43# wakati akihojiwa na Channel 10  ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Sijaona Simon.
Afisa Masoko Msaidizi wa Access Benki, Humphrey Masudi akiwaomba watanzania wateja wa benki hiyo kuitumia kikamilifu huduma ya 'RAHISI' inayomsaidia mteja kuweza kutoa na kuweka pesa popote alipo kupitia simu yake ya mkononi... piga *150*43# wakati akihojiwa na Channel 10  ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Access Benki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelewa na Kamera ya Kajunason Blog.
Wafanyakazi wa Access Benki wakisuburi kuhudumia wateja.
Kila mmoja akiweka mambo sawa....
Afisa Masoko Msaidizi wa Access Benki, Humphrey Masudi akiulizwa swali na mmoja ya wateja aliyetembea bandani kwao.

SAMAHANI KWA PICHAZ HIZI: NDIO TULIPOFIKA WATANZANIA

$
0
0
Kweli Bongo Movies Sasa Inakwenda ‘Next Level’ 
Hizi ni picha za nyuma ya kamera za moja ya filamu ya kibongo ‘Bongo Movies’ ambapo msanii Haji Adam ‘Baba’ amevaa uhusika kwa kuwa na majeraha usoni. Hizo ni make up tu. Hakika Bongo Movies sasa zimeanza kubeba uhalisia. Hongeren sana.
 




DIAMOND PLATINUMS ATEULIWA KUINGIA KWENYE TUZO NYINGINE UGANDA

MTOTO MDOGO AVUNJA PROTOKO ZA JESHI..

$
0
0
Hali ya hisia kali ilikumba hadhira iliyokwenda kuwapokea wanajeshi wa Marekani waliotoka Afghanistan baada ya kutumikia jeshi wakiwa huko kwa miezi tisa kabla ya kuungana na familia zao. 
Wakati wanajeshi hao wakipokea amri ya jeshi kabla ya kuruhusiwa kukutana na familia zao mtoto wa miaka mitatu Cooper Waldvogel uvumilivu ulimshinda na kukatiza kumkimbilia.

Bila ya kujali protokali mtoto huyo aliwaponyoka watu waliokuwepo na kukimbilia moja kwa moja mikononi mwa mama yake na kumkubatia kwa hisia kali.

KWA HALI HII AJALI ZA BODA BODA HAZIISHI

MAMBO YA AIBU YANAYOFANYWA KENYA

THE MAGAZETI YA BONGO LEO SUNDAY /JUMAPILI 05/7/2015 LIVE!!


KWA WALE WADADA MAMBURULAA WA MJINI MNAOPENDA KUIGA, IGENI NA HII SASA KAMA MNAWEZA!!

BIDHAA BORA ZA FELTRON ZIMEINGIA NCHINI RASMI

$
0
0

Jipatie bidhaa bora na halisi kwa ajili ya majumbani na maofisini kutoka kampuni ya Feltron ya
Falme za Kiarabu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Wakala rasmi nchini:
F- Zone (T) Ltd
web site: www.fzone.com

DIAMOND PLATINUMS ATEULIWA KUINGIA KWENYE TUZO NYINGINE UGANDA

$
0
0


SUPER STAR DIAMOND PLATINUMS AFICHUA SIRI KUHUSU AY

$
0
0

Msanii supastaa wa bongofleva Naseeb Abduli “Diamond Platnumz” amefunguka jambo muhimu sana kuhusu nyota mwingine wa bongofleva ‘long time’ AY. 
Diamond kupitia ukurasa wake wa facebook amebainisha kuwa AY ndiye aliyemfungulia njia ya kung’ara kimataifa. Diamond alikuwa akiyasema hayo wakati akimtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa.  

KUMBE DIAMOND ALIFANYA NYIMBO ISHIRINI KABLA YA KUTOKA!

$
0
0
 
Diamond kabla ya mafanikio.
Kampuni ya Coca-Cola Afrika ya Kati, Mashariki na Magharibi imezindua kampeni mahsusi ijulikanayo kama ‘Sababu Bilioni za Kuamini’ inayolenga kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kujiamini pindi wanapopita katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kimaisha kabla ya kutimiza ndoto zao. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itaendeshwa nchi nzima.
Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ni miongoni mwa vijana wanaotolewa mfano katika dhana hii. Alitengeneza single zaidi ya 20 kabla ya kufanikiwa na hatimaye kufikia katika mafanikio makubwa aliyonayo sasa
Mwaka 2007 Diamond alifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuza mitumba, kufanya kazi katika vituo vya kujaza mafuta pamoja na kupiga picha mitaani ili aweze kupata fedha zilizohitajika studio.


 Diamond Platnumz
Hata hivyo, hakukata tamaa na ni kutokana na moyo wake huo wa kutokubali kushindwa kwa urahisi ameweza kufanikiwa na kuwa miongoni mwa nyota wachache wa muziki anayetamba aliye kijana tajiri mkubwa kwa sasa hapa nchini.
“Kupitia kampeni hii, Coca-Cola itaweza kuwaletea simulizi zaidi juu ya mafanikio ya watu ambao hawakukata tamaa licha ya kutofanikiwa mara kadhaa katika safari zao za kuelekea kwenye mafanikio. Sababu zilizowafanya wasikate tamaa ni kutokana na imani yao kuwa kuna siku ambayo wangekuja kufanikiwa. Na hicho ndicho tunachotaka vijana wa Kitanzania waweze kuiga. Wawe na moyo wa kutokata tama licha ya kukumbana na changamoto nyingi katika safari yao kuelekea katika mafanikio,” Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka.
Coca-Cola imewekeza katika programu ya soka kwa vijana ijulikanayo kama Copa Coca-Cola ambapo vipaji vya wachezaji nyota kama vile Thomas Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya nchini Congo na mfungaji bora wa ligi kuu nchini Simon Msuva anaechezea Yanga vimeweza kuibuliwa na Copa Coca-Cola. Vile vile Coca-Cola inasaidiia kuinua wanamuziki wa Tanzania kupitia programu ya Coke Studio. 
 Simon Msuva
Thomas Ulimwengu
Katika kipindi hicho cha kampeni, Kampuni ya Coca-Cola itakutana na kuwafikia kwa karibu zaidi vijana shuleni na maeneo mengine wanakoishi ili kuwawezesha kutambua uwezo walionao katika kufanikisha maisha yao. Itawawezesha kusimulia hali halisi ya maisha yao na ndoto wanazokusudia kuzifanikisha katika maisha. “Coca- Cola inatumia kampeni hii kuwahamasisha na kuwajengea uwezo ninyi vijana wa Kitanzania muweze kujiamini kutokana na uwezo mlionao katika dunia tuliyomo ambayo mambo yasiyo na uhakika yanazidi kuongezeka,” alisema Njowoka.
Kampeni ya Sababu Bilioni za Kuamini (Billion Reasons to Believe- BRTB) inalenga kuwafanya vijana wajiamini na kutoyumba katika kuzifikia ndoto walizojiwekea licha ya mara kadhaa kukumbana na changamoto zilizowafanya kutofanikiwa kila walipojaribu katika hatua za awali. 
Sababu Bilioni za Kuamini ni kampeni inayoendeshwa kwa njia mbalimbali ambazo ni pamoja na TV, radio, matumizi ya njia za kidigitali na matangazo ya nje ikiwa ni pamoja na shughuli za maonyesho ili kuwezesha ushiriki wa watu wengi nchi nzima.

HAWA NDIO WANAUME WALIOJIBADILISHA JINSI NA KUWA WANAWAKE...CAITLYN JENNER AJIUNGA CHAMA CHAO RASMI!

$
0
0

Baba wa kufikia wa Kim Kardashian, Bruce Jenner, Caitlyn Jenner.New York Marekani
Baba wa kufikia wa Kim Kardashian, Bruce Jenner, ambaye kwa sasa amekuwa mwanamke akifahamika kwa jina la Caitlyn Jenner juzi kati alienda kukutana na wanawake tata wenzake ikiwa ni utambulisho rasmi toka aingie kwenye chama chao cha kutoka mwanaume na kuwa mwanamke.


Utamburisho huo ulifanyika kwenye sherehe ya chakula cha usiku iliyoandaliwa maalumu mjini New York ambapo Caitlyn alionekana kuwafunika wenzake kwa kupendeza zaidi.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja nchini humo; “Haijulikani ni upya wa muonekano wake ama la lakini Caitly alionekana kupendeza hasa kwa nywele zake alizoziachia na kuwafunika wenzake wote waliokuwa eneo la sherehe”,  

HUYU NDIO MKE WA MWANAMUZIKI TAJIRI JOSE CHAMELEONE WA UGANDA!

$
0
0


Mwanamuziki mkongwe na anayetajwa kama tajiri zaidi Afrika masharika Jose Chameleoneakiwa na mkewe na picha za juu nyingine wakiwa na familia yao katika matukio tofauti!
Unayaonaje maisha haya mdau?!

TEAM WASIRA NA URAIS 2015

$
0
0
Tovuti ya Wasira 2015 - Tovuti hii inajumuisha habari mbalimbali za Mh. Stephen Wasira  akiwa katika safari yake ya kutafuta wadhamini ili kupata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi ujao. Safari hii ilimfikisha mikoa 31 nchini kote Bara na Visiwani.
Bofya hapa kuona Video, picha na mengineo www.wasira2015.co.tz

ALIYEWALOGA HAWA WAREMBO KAFA,JIONE WANAVYOVAA

SUPER STAR DIAMOND AFANYIWA KUFURU NIGERIA

$
0
0

Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Pasua anga! Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefanyiwa kufuru ya bonge la pati na msanii mwenzake kutoka nchini Nigeria, Kingsley Chinweike Okonkwo ‘KCEE’ Ijumaa Wikienda lina ubuyu kamili.Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichosafiri na staa huyo ambaye yupo nchini humo kwa ziara yake inayofahamika kama ‘Nana Tour’, tangu Diamond alipofika siku ya kwanza akiwa na mameneja wake, Salam, Babu Tale, DJ wake aitwaye Romy Jones na wengine, mastaa kibao wakubwa walikuwa wakihitaji kuwa wenyeji wake.
“Jamaa ana uhusiano mzuri sana na mastaa wa Nigeria. Kuna ambao ameshafanya nao kazi kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Bracket, Iyanya, KCEE na P Square (bado haijatoka). “Pia wapo wengine kibao wanaotaka kufanya naye kazi hivyo wanamuwinda.
Waliposikia anakuja kufanya ziara ya wimbo wake mpya kila mmoja alitaka kuwa mwenyeji wake. 

MWEZI MTUKUFU,FUTARI YAZUA BALAA!

$
0
0
Akihojiwa baada ya kuminyiwa kichapo. 
 Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Asha, mkazi wa Mtaa wa Area Six, Kata ya Kichangani mkoani hapa ambaye alikuwa kwenye swaumu ya Mfungo wa Ramadhani, amejikuta akilazimika kutengua swaumu na kumpa kichapo mwanaume aliyeiba futari na kiti chake cha plastiki alichokuwa amekalia nje ya nyumba akipika futari hiyo.

Tukio hilo la aina yake, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wakati paparazi wetu anawasili kwenye eneo la tukio, alikuta kasheshe bin tafrani ikiendelea. Mbali na mwanamke huyo, wananchi wenye ghadhabu nao walikuwa wakimshikisha adabu mwanaume huyo huku wakidai ni mwizi. 


BOFYA KUONA PICHA ZAIDI

ROSE MUHANDO APIGWA PINGU DOM, ASAFIRISHWA DAR

$
0
0



TOO much! Kufuatia skendo ya utapeli inayoendelea kumwandama mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kupigwa pingu mkoani Dodoma, baadaye akasafirishwa hadi Dar kwa msimamizi wa kazi zake, Alex Msama, kwa lengo la kumlipia deni alilokuwa akidaiwa, Ijumaa Wikienda lina kisa chote.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando.
Habari kutoka kwa chanzo zimeeleza kwamba, hivi karibuni, Rose alilipwa Sh. milioni 3 kwa ajili ya shoo huko Makambako mkoani Njombe na matangazo yakafanyika lakini hakutokea.
Ikadaiwa kuwa, wakati matangazo ya shoo yakiendelea, mtu mwingine aliyekuwa akimdai Sh. milioni 3.5 (pia alichukua fedha kwa shoo siku za nyuma) alikwenda Makambako kwa lengo la kumsubiri Rose ili amnase, lakini hakutokea.
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘unyunyuzi’ kuwa, wawili hao waliripoti ishu ya Rose, Kituo cha Polisi Makambako ambapo polisi walifunga safari kumfuata Dodoma.
Sosi huyo alisema kuwa, Rose alikamatwa Juni 27, mwaka huu na kuswekwa rumande Kituo Kikuu cha Polisi, Dodoma tayari kwa kupelekwa mahakamani. Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake.
“Msama alikubali kwa sharti kwamba, kwa sababu ana kazi ya kufanya na Rose hivyo asafirishwe hadi Dar amlimpie, yeye na Rose watakatana kwenye kazi.
“Rose alisafirishwa Juni 29, mwaka huu akiwa chini ya ulinzi wa askari wawili. Mmoja wa kike ambaye alilala naye chumba kimoja hotelini. Kesho yake wakaenda ofisini kwa Msama, Block 41, Kinondoni, akalipa milioni sita na laki tano keshi,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyetishiwa skendo hiyo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Msama ambapo alidai waulizwe wafanyakazi wake.
Mmoja wa wafanyakazi wake aliyeomba hifadhi ya jina, alikiri Msama kumlipia Rose kiasi hicho cha pesa.
“Ni kweli! Rose aliletwa hapa toka Dodoma chini ya ulinzi wa polisi wawili. Msama akamlipia shilingi 6,500,000 ambazo watakatana kwenye kazi zao,” alisema mfanyakazi huyo.Rose alipotafutwa, Alhamisi na Ijumaa iliyopita, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>