1.UHURU
-Tanganyika Ilipata Uhuru kwa dharula. Zanzibar ilifanya mapinduzi kwa dharuala.
2.MUUNGANO
-Muungano wetu ulifanyika kwa dharula. Ndio maana mpaka leo umegubikwa na mizengwe.
-Tuliletewa hati ya muungano ya A4 wakati karatasi za saizi hiyo hazikuwapo miaka ya zamani ni Dharula
3. SIASA NA VYAMA
-Chama tawala kiliundwa kwa dharula. Ndio maana kuna matabaka mpaka leo.
-Vyama vingi viliingia nchini kwa dharula. Hatukuwa tumejiandaa bali yaikuwa ni matakwa ya Wakoloni.
-Viongozi wa vyama vyote hupatikana kwa dharula.
-Kiongozi akiharibu sehemu Fulani hupelekwa sehemu nyingine akaharibu kwa dharuala
4. ELIMU
-Elimu yetu ni ya dharula. Utakubaliana na mimi tu fikiria “Crash programe ya walimu , Shule za kata zimejegwa kwa dharula ndio maana hazikuwa na walimu, madawati, vitabu, vyoo na zaidi yayote maabara , nyumba za walimu na maradh
i kwa walimu ni ya dharuala.
-Ufaulu ni wa dharuala. Wanafunzi wakifeli, huongezewa viwango vya ufaulu kwa dharula.
-Wanafunzi wa elimu ya juu siku hizi wakimaliza elimu zao hupata kazi kwa dharula tu kwa sababu mfumo wa elimu ni wa dharula tu haumuandai kijana katika kujiajiri mwenyewe.
5. AFYA
-Madaktari wakigoma ni dharula kwani tunaambiwa jeshi linao madaktari wa kutosha kutoa huduma nchi nzima.
-Dawa zikiwa feki tunaambiwa zilipitishwa kimakosa na TBS ama palitokea dharula.
-Huduma za afya mbovu ni dharula kwani serikali inajitahidi sana.
-Vifo vya mama na motto vikiongezeka ni dharula.
-Kufanyiwa oparesheni kichwani badala ya mguuni ni dharula kwani manesi wamechanganya mafaili.
-Maralia, Ukimwi na Kansa bado ni dharula kwani jitihata za kuyatokomeza zinafanikiwa sana.
6. HUDUMA NYINGINEZO
-Umeme unakatika katika kwa dharula na Mgao ni wa dharula ndio maana nchi nzima haijawahi kuwa GIZA sio kwamba Tanesco wameshindwa kazi (*Majibu ya Waziri* 1999.)
- Maji safi na salama ni shida kwani hutengewa bajeti kwa dharula (*Majibu ya Waziri* 2010.)
7. SHERIA MBOVU
-Katiba ilitungwa na wananchi ili wakaikataa ikaletwa ya dharula na kuungwa mkono.
-Sheria hupitishwa kwa dharula, tumeona yaliyotokea bungeni kuanzaia wiki iliyopita mpaka jana.
8. MIUNDO MBINU
-Barabara mbovu kwani hutengenezwa kwa dharula kipindi uchaguzi ukikalibia.
-Bomoa bomoa ni za dharula kwa sababu viwanja havipimwi kwa wakati.
-Mifereji michafu, kwa sababu watu hutupa taka kwa dharula wakati wa usiku.
-Mafuriko hutokea kwa dharula pindi maji yanapokosa mwelekeo. Hii ni kwa sababu viwanja huuzwa kwa dharula sehemu za mabondeni.
9. MIGOGORO YA ARDHI
-Wazawa kugombea Ardhi kwa sababu Ardhi imeuzwa kwa dharula kwa wawekezaji wan je.
-Vurugu mpaka kuuana bado ni za dharula haziwezi kuzuiliwa.
-Watu kudhurumiwa Ardhi zao ETi ! mkuu wa wilaya anawahadaa na kuwambia shule na makazi havita vunjwa ni dharula tu(*Jana Arumeru.*ITV)
10. MAUAJI
-Mauaji ya ndugu zetu Albino serikali imeshindwa kuwadhibiti wahusika kwa sababu hutokea kwa dharuala bila ya wao kujua.
-Mauaji ya vikongwe ni dharula, serikali inakuwa haijajiandaa.