Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

VILIO NA MAJONZI SINGIDA WAKATI MO AKIWAAGA WANANCHI WAKE!

$
0
0
IMG_7558
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.
Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB) wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.

Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo elimu na Afya
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo." alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini" alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1,000.
IMG_7562 
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema
Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida mjini.
Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza bungeni.
Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.
Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10, unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 81.
Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi chote!
IMG_7530
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza kutogombea tena.
Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba: "kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake, ikiwemo mimi mwenyewe."
Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.
"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.
"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! "
IMG_7549
Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake huku machozi yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.
IMG_7533
Watoto hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la ubunge wa Singida mjini.
IMG_7533IMG_7535
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
IMG_7536IMG_7567
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya People's Club.
IMG_7402
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa Singida mjini.
IMG_7588
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo.
IMG_7428
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake wakishambulia jukwaa.
IMG_7440
IMG_7445
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya Diamond Platnumz.
IMG_7447
IMG_7453
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika viwanja vya People's Club, Singida mjini.
IMG_7454
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
IMG_7471
IMG_7476
IMG_7478
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
IMG_7481
Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika katika viwanja vya People's Club kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh. Mohammed Dewji.
IMG_7610
IMG_7617
IMG_7626
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
IMG_7629
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
IMG_7642
IMG_7633
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa wananchi wa Singida mjini.
IMG_7645
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
IMG_7675
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
IMG_7712
Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
IMG_7716
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia) akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses Iyobo.
IMG_7728
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
IMG_7735
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.

BREAKING NEWS YA MAPENZI,AUNT EZEKIEL AJICHORA JINA LA DANCER WA DIAMOND PLATNUM NA MWANAE.

$
0
0

Bongo movie Aunt Ezekiel mapenzi ya dancer wa Diamond yamdatisha hadi kufikia hatua ya kujichora mwilini jina la mpenziwe huyo Moses Iyogo,Na jina la mtoto wao Cookie.Aunt Ezekiel miaka ya karibuni amechukua maamuzi
magumu ya kutulia kwenye mapenzi ingawa aliolewa na haieleweki ndoa hiyo ilikuwa na hatma gani.Wapenzi ambao wamejichora majina ya wenza wao nipamoja na Nuh Mziwanda, bila kusahau mpenzi mpya wa Linah.  

BOFYA KUONA PICHA ZAIDI

DIAMOND ASEMA YUPO TAYARI KUFANYA COLLABO NA MSANII YEYOTE TANZANIA ILI MRADI AWE NA VIGEZO!

$
0
0

Diamond Platnumz amesema kuwa yuko tayari kufanya collabo na msanii yeyote wa Tanzania, ambaye atakuwa anakidhi vigezo vyake.
Muimbaji huyo wa ‘Nana’ ameyasema hayo baada ya kuulizwa kwanini hafanyi collabo nyingi na wasanii wa Tanzania.

“Mimi sina tatizo as long as nijue hiyo kazi unayotaka kufanya na mimi itafika wapi,”alisema Diamond kupitia Clouds FM.
“umejipanga vipi project yako na umeiandaa vipi, kwasababu sitaki nifanye tu nyimbo mwisho wa siku halafu iishie tu ndani unaiskiliza wakati natumia muda kukaa kuandika kupoteza muda studio.“  

NANI WAKUSHINDANA NA DIAMOND PLATNUM.

$
0
0
SHUGHULI YA LEO SINGIDA MH DEWJI AKITANGAZA MAFANIKIO YA JIMBO NDANI YA MIAKA MITANO.MWENYEKITI WA ACT ANNA MGHWIRA ANATARAJIA KUTANGAZA NIA JIMBO HILI KUNA USHINDI KWELI ACT.

PICHA DIAMOND PLATINUMS ALIVYOSHEREKEA SIKU YA KUZALIWA MAMA YAKE

VITUKO UCHAGUZI MKUU 2015: STEVE NYERERE AAJIRI MLINZI

$
0
0
Msanii wa filamu Bongo, Steven Mengere, ‘Steve Nyerere'. Chande Abdallah
MAKUBWA HAYA! Msanii wa filamu Bongo ambaye ameingia kwenye listi ya waliotangaza nia kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kinondoni, Steven Mengere, ‘Steve Nyerere’ amedaiwa kuajiri mlinzi wake binafsi ili kujihami na maadui wake wa kisiasa.
Steve alinaswa na paparazi wetu akiwa analindwa na ‘bodigadi’ kila alipokuwa akienda ndani ya Viwanja

vya Leaders Club, Dar kulikokuwa na hafla ya uchangiaji waandishi wa habari, Media Car Wash na aliweka wazi kuwa hiyo yote imetokana na uamuzi wake wa kuingia kwenye siasa.
“Nimeambiwa na wazee kuwa nisiwe peke yangu, si unajua tumeingia upande wa siasa, ni mambo ya kiusalama zaidi ndiyo maana nimemwajiri huyu,” alisema Steve Nyerere baada ya kuulizwa kuhusu suala hilo.

MSICHANA ANAYEMZIMIKIA DIAMOND AIBUKA NA KIOJA CHA MWAKA

$
0
0
Watanzania munisuport Mimi Tanzania mwenzenu...... uyo Mgandaa ni 360 watanzania wotee ni nduguu mali za watanzinia zitumiwee na wataniaa iwejee MTU from no where atuchukulie kijana wetuu mnajua Tanzania hairuhuruu urai wa nchi mbili what if diamond akiamua
kufunga ndoa na zari Diamond akachukua Uraia wa South ili wamlee mtoto hamuoni atakua tumepoteza icon... muni support nimpate dai tuoanee atabakia kwetu..... nipigieni kura Mumtagg Diamond najua akiniona niko natural atanitongoza.... 


PICHA WAGOMBEA URAIS WAKIWA NJE YA CHUMBA CHA KUSUBIRIA MAJIBU


KILICHOJIRI KWENYE KIKAO CHA DODOMA , RAIS KIKWETE ANENA MAZITO LIVE

$
0
0
Siasa zinapewa nafasi kubwa sana sasa hivi, Tanzania inaingia kwenyeUchaguzi Mkuu Mwezi October 2015… Tayari wapo waliotangaza Kugombea nafasi mbalimbali lakini macho ya wengi yako kwenye nafasi ya Urais, mpaka sasa kuna majina
zaidi ya 35 ya watu waliotangaza Kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM.
Rais Kikwete yuko Dodoma, imenifikia hii Ripoti ya kilichoendelea jana wakati wa Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili cha CCM.  

DIAMOND, ZARI KIMENUKA MBAYA! DIAMOND AHAHA, ZARI AJUTA, MIMBA YAWA KIKWAZO, OMOTOLA ATAJWA!

$
0
0
Nasibu Abdul ‘Diamond akiwa na Zari.
OHOOO! Wakati penzi lao likitarajia matunda ya kupata kijacho miezi kadhaa ijayo, uhusiano wa Nasibu Abdul ‘Diamond na staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ umedaiwa kutibuka baada ya Diamond kufunguka kuwa anampenda mwigizaji wa Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde, Amani linakupa mchapo.


Mkali wa Bongo fleva Nasibu Abdul ‘Diamond.Diamond aliitoa kauli hiyo hivi karibuni jijini Lagos alipokuwa akihojiwa redioni ambapo alipoulizwa ni wasanii gani maarufu anavutiwa nao kimapenzi, bila hiyana, mkali huyo kutoka Tandale-Dar, alisema ni Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji. 


BONYEZA HAPA KUJUA KISA CHOTE

TANO BORA YA URAIS CCM ITATOKA NDANI YA KUNDI HILI MAJINA YAO HADHARANI LEO,33 KWENDA NA MAJI

$
0
0
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya RaisKamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo inakutana kuchuja majina ya makada wake 38 waliorejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho na majina 33 ni lazima yapigwe panga ili kupeleka majina matano kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupigiwa kura.
Kwa mujibu wa habari kutoka mitandao ya kijamii, kwenye vijiwe na mijadala sehemu mbalimbali, majina hayo matano yanaaminika kwamba yatatoka miongoni mwa watiania 10 ambao wametajwa zaidi katika mijadala hiyo.
Sababu kuu mbili ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye mijadala hiyo na hata na baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa Tanzania ni mbili. Mosi, uzoefu wao ndani ya ungozi wa serikali na pili, nafasi yao ndani ya chama, ama kama wajumbe wa NEC au Kamati Kuu.  

BONYEZA HAPA KUONA KUNDI LA KIFO

THE MAGAZETI YA BONGO LEO THURSDAY /ALHAMISI 09/07/2015 LIVE!!

$
0
0



 


.













.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.




.








.


AY

PICHA WEMA SEPETU WAFUTURU PAMOJA NA VJ PENNY

$
0
0



After diamond Saga ended Now Wema sepetu and Vj penny their friendship become more strong spotted in different places together even in Ramadan!! Must see PHOTO'S.


 


MZEE KINGUNGE ATOA YAKE YA MOYONI MJINI DODOMA

$
0
0

MWANASIASA mkongwe nchini, mzee Kingunge Ngombale Mwiru, amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutofanya dhihaka ya kumpendekeza kada yoyote kuwa mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwani kwa kufanya hivyo kitaanguka.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Julai 8, 2015, Kingunge ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini
na ndani ya chama hicho alisema “ninatishwa na watu wanaotumia nguvu nyingi kwelikweli kupambana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, badala ya kuelekeza nguvu hizo kupambana na wapinzani wetu, hii ni hatari.’, alionya
Amesema, CCM ni lazima ifuate katiba yake ili wajumbe wanaotarajiwa kutoa maamuzi watoe maamuzi sahihi na sio kupindisha katiba kwa kuanzisha utaratibu ambao sio utamaduni wa kidemokrasia.
“kuna kiongozi mmoja anasema, kada yeyote wa chama hicho aliyeomba kuteuliwa kuwania urais, endapo jina lake litakatwa hatakuwa na nafasi ya kukata rufaa, hii haijawahi kutokea na wala haipo kwenye katiba yetu.’ Amesema Mzee Kingunge.
"CCM lazima imteue mtu anayekubalika ndani na nje ya chama ili chama kiweze kushinda, kinyume na hapo, hii ni njama ya kukifanya kishindwe kwenye uchaguzi".

Hivi karibuni Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa hakutakuwa na nafasi ya kada wa chama hicho atakayeenguliwa kwenye mchujo kuweza kukata rufaa, kwani hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.

Hata hivyo Kingunge amepinga kauli hiyo na kusema, inakwenda kinyume cha katiba ya CCM ambayo inaweka bayana kuwa maamuzi ya vikao vya chini yanaweza kukataliwa na vikao vya juu ikiwa ni pamoja na mwanachama ambaye anaona hakutendewa haki kuwa na nafasi ya kupinga uamuzi wa vikao vya chini.

DIAMOND PLATNUM AMALIZA BIFU NA PRODUCER MANEKE BAADA YA KUVUJISHA NYIMBO

$
0
0

Bifu kati ya msanii Diamond na mmiliki wa studio ya AM record Maneke wamelimaliza rasmi nakufanya kazi mpya.Bifu hilo lilizaliwa miaka miwili nyuma
sababu nikuvujishwa nyimbo ya ukimwona.Nyimbo hiyo mpya anamshirikisha Ney wa Mitego.Mwezi wa ramadhan na neema zake.

HUYU MREMBO LEO KAZUA GUMZO MTAANI KWA NGUO ZAKE

$
0
0
 

See full video below...Tazama video hapa chini!

NAPE HATIMAYE AFUNGUKA KUHUSU MCHAKATO UNAOENDELEA KWENYE UTEUZI WA URAIS CCM

$
0
0

Hatimaye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM)Nape Nnauye ameongea na waandishi wa habari asubuhi ya hii ya saa 3 kuhusu mchakato wa kuteua mgombea wa Urais kupitia chama cha CCM unaoendelea Dodoma.
Nape Nnauye amesema kwamba siku ya juzi na jana hakikufanyika kikao chochote kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali ila vikao vitatu muhimu vitafanyika siku ya leo. 

FAMILIA ZA WAGOMBEA URAIS CCM VILIO VYATAWALA . DODOMA SI MCHEZO!

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM, rais Jakaya KikweteSi mchezo! Baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia na kuridhia majina matano ya wanachama wake walioomba kuteuliwa kuwania Urais katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, baadhi ya familia za wagombea hao zilizo mjini hapa zimejikuta zikiangua vilio huku zile za waliopenya TanoBora ziliripuka kwa furaha. Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa familia mbili za wagombea tofauti zilizofikia katika hoteli moja yenye hadhi iliyo mjini hapa, zilijikuta zikiungana kwa furaha baada ya kubaini watu wao wamepenya katika hatua hiyo ngumu ya uteuzi. 

BREAKING NEWZZ!!:- MBUNGE WA ZAMANI WA CCM AFARIKI DUNIA!!

$
0
0
 
Tunapenda kuwajulisha kifo cha ghafla cha aliekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini CCM 1995-2005, Mzee Leonard Newe DEREFA, kilichotokea mapema leo asubuhi 09.07.2015 Nyumbani kwake Shinyanga Ngokolo, mjini.
Tunapenda kutoa pole za dhati kwa Familia na chama chake cha CCM.Taarifa zaidi Tutawajuza hapa. BWANA alitoa na BWANA ametwa, Jina lake libarikiwe. RIP Mwana Derefa.
Mazishi yanategemewa kuwa siku ya Jumapili tarehe 12.07.2015 Shinyanga Mjini.

TANO BORA CCM URAIS: HIKI NDICHO KILICHOJIRI KATIKA KIKAO CHA

$
0
0
Kila mmoja anayo shahuku ya kujua majina 5 yaliyopitishwa na kamati kuu iliyopangwa kukukatan jana usiku mjini Dodoma.
Taarifa rasmi zilizotufikia  kutoka Dodoma ni kuwa kikao hicho kiliketi na kuhahirishwa hadi leo asubuhi kutokana na sababu ambazo hazijatajwa rasmi.
Taarifa ya CCM ni kuwa leo ijumaa kutakuwa na vikao viwili ambapo kitaketi cha wanza kupata wateule watano na baadaye halmashauri kuu kukutna na kuteua watatu miongoni mwao ili majina hayo yapelekwe kwa mkutano mkuu hapo kesho.   

BOFYA HAPA KUONA BAADHI YA MAJINA YALIOPENDEKEZWA KUINGIA 5 BORA
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>