Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

MFAHAMU MKE WA MGOMBEA JOHN POMBE MAGUFULI.


WASIFU WA JOHN POMBE MAGUFULI.

$
0
0
John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 huko wilayani Chato Mkoani Kagera (hivi sasa Chato ni wilaya ya mkoa mpya wa Geita) na atatimiza miaka 56 Oktoba mwaka huu.Kisha alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai - Desemba 1983), kisha akaenda kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari hadi Machi 1984) na akamalizia katika kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984).

Mwaka 1985 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988.
Mwaka 1989 - 1995 alifanya kazi katika kiwanda cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.) akiwa mkemia na wakati huohuo alianza masomo ya shahada ya uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza, kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisoma kati ya mwaka 1991 na 1994.
Magufuli aliendelea na elimu ya juu zaidi kwa maana ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia kuanzia mwaka 2000 hadi 2009 ambayo aliihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa mhitimu wa shahada ya udaktari. Dk Magufuli ana mke, watoto na familia imara.

Jambo jingine linaloweza kumvusha Magufuli ni msimamo. Yeye ni kiongozi mwenye misimamo isiyotia shaka. Hajui kuuma maneno lakini anajua nini anachokisimamia. Watendaji wa Wizara ya Miundombinu wanasema ni vigumu kumyumbisha Magufuli katika jambo ambalo anaona hilo ndiyo njia, lazima mlitekeleze kwanza. Tabia ya namna hiyo alikuwa nayo Mwalimu Julius Nyerere, kwamba akishaamua jambo fulani na kama anajua njia yake, humtoi relini.

WASIFU WA ASHA ROSE MIGIRO,NA FAMILIA YAKE MUME NA MABINTI ZAKE WAWILI.

$
0
0
Asha-Rose Mtengeti Migiro Amezaliwa 1956 aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Amepewa cheo hiki naKatibu Mkuu Ban Ki-moon tar. 5 Januari 2007.
Hadi kuteuliwa kwa cheo cha UM alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kumfuata katika wizara ya mambo ya nje iliyoshikwa awali na Kikwete mwenyewe.
Chini ya raisi Benjamin Mkapa Migiro alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa mbunge kwa njia ya kiti maalumu cha wanawake.
Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alisoma digrii za bachelor na master Dar es Salaam. Mwaka 1992 akaongeza cheti cha udaktari wa sharia kwenye Chuo kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Akarudi Tanzania alipoanza kufundisha. Akawa mwanachama wa CCM
Akiwa Mwislamu ameolewa na Cleophas Migiro wana watoto wawili wa kike.
 Dkt. Asha Rose Migiro a waziri wa katiba na sheria wa Jamuhuri ya muungano TANZANIA


WASIFU WA MGOMBEA TATU BORA BALOZI AMINA SALUM.

$
0
0
       Balozi Amina alidumu kwa muda mrefu kama waziri kwenye serikali ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour Juma, aliwahi kutupa karata yake kuwania urais wa Zanzibar, kabla ya kujitoa.
              Huyu anakuwa mwana mama wa kwanza kwenye historia ya chama cha Mapinduzi CCM, kutangaza kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hali kadhalika, Balozi Amina rekodi yake ya kwanza ni kuwa mwanamke wa kwanza kuwa balozi wa kudumu wa AU huko Marekani.
                       Mbali na kuwahi kuwa waziri, Balozi Amina ndiyo muasisi wa taasisi ya Zanzibar Women Welfare Trust, inayojishughulisha na kupambana na afya ya akina mama na watoto hususan kwenye eneo la maambukizi ya VVU.

Kitaaluma Amina anayo shahada ya uchumi.


MATOKEO YA MGOMBEA URAIS KUTANGAZWA KESHO SAA NNE ASUBUHI.

DIAMOND PLATNUM ASEMA WEMA ANGEJUA JINSI ZARI ANAVYOPENDWA ANGEJIFUKIA.

$
0
0
ATEMA KIMOMBO ''I WISH YOU CAN UNDERSTAND HOW MUCH I LOVE THIS WOMAN,THANKS GOD FOR THE LIFE HAVE ALWAYS PRAYED FOR......'' AKIMAANISHA TAJA JINA LA SEHEMU ILIYOACHWA WAZI!!

LOWASSA AWA LULU KWA WAGOMBEA WENGINE DODOMA...TAZAMA HALI ILIVYOKUA DODOMA!

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, leo katika Ukumbi wa jengo la White House mjini Dodoma. Kikao hicho ni cha kuchagua wagombea watatu kati ya watano waliopitishwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kuwania kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Watatu watakaopatikana leo, watapelekwa kuigiwa kura katika Mkutano Mkuu wa CCM ili kupata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mkuu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utanguzi kumkaribisha Kikwte kufungua mkutano huo. Kushoto ni Dk. Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao hicho 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto_ alipoingia ukumbini. Waliosimama mbele ni Wajumbe waalikwa wa kikao hicho kutoka Baraza la Ushauri la Wazee Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi na Benjamin William Mkapa na wengine ni Makamu Wenyeviti wastaafu Mzee John Malecela na Mzee Pius Msekwa
Kikao hicho kikiendelea
YALIYOJIRI KABLA YA KIKAO HICHO
Aliyekuwa muomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameenguliwa, Edward Lowassa akiwasili kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM kuhudhuria kikao cha NEC.
Lowassa akiingia ukumbini 
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Mzee Msidai akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho cha NEC
Mjumbe wa NEC, Dk. Chegeni akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, wa CCM, Zakiah Megji akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Steven Wasira akifuatwa na Waandishi wakati akiingia ukumbini
Kada wa CCM kutoka Zanzibar, Mohamed Raza akizungumza na waandishi ambapo aliipongeza Kamati Kuu ya CCM kwa kuweza kufanya uteuzi wa watu watano na kueleza kuwa inabidi waliokosa kuteuliwa wawe watulivu kwa kuwa ndiyo Demokrasia
Muomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Bernard Membe ambaye amefanikiwa kuingia tano bora, akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho leo
Muomba kuteuliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameingia tano bora, John Magufuli, akimsikiliza kwa makini mmoja wa wajumbe wa NEC, aliyekuwa akimnong'oneza jambo kabla ya kuingia ukumbini
Waomba kuteuliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM ambao wamefanikiwa kuingia tano bora, Januari Makamba na John Magufuli wakicheka kwa furaha walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kuingia kwenye kikao hicho. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Januari Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora waliokuwa nje ya ukumbi wakati wa kikao hicho
Wakuu wa vyombo vya habari vya CCM, Angel Akilimali (Uhuru FM) na Ramadhani Mkoma (Uhuru Publications Ltd
Muomba ridhaa ya CCM kuwania Urais Bernard Membe akiwasalimia wajumbe ukumbini pengine kuomba kura zao kabla ya kuanza kikao hicho
Waomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, ambao wamefanikiwa kuingia tano bora Bernard Membe na Dk. Asha Rose Migiro wakisalimiana ukumbini wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Samwel Sitta ambaye pia aliomba nafasi hiyo lakini hakuingia tano bora
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Lazaro Nyalandu ambaye hakuingia tano bora, akizungumza na Adam Malima
Wajumbe wakiwa ukumbini
"Usijai kaka" Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM kuwania Urais, Mwiguku Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.
"Usijai kaka" Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM kuwania Urais, Mwiguku Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Edward Lowassa ambaye hakpita tano bora, wakati wa kikao hicho.
"Naomba kura yako Ndugu yangu" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho.
"Naomba kura yako Ndugu yangu" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho
"Naomba kura yako Ndugu yangu, tena napiga magoti" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho
January Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa wakati wa kikao hicho cha NEC
Membe na Januari Makamba wakisalimiana ukumbini
Baadhi ya wajumbe ukumbini
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mzee Sitta wakati wa kikao hicho cha NEC
Dk. Asha-Rose Migiro ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa na kumuomba kura wakati wa kikao hicho cha NEC leo
Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti wakiwa kwenye kikao hicho
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kikao hicho cha NEC

SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO PIA YAZINDUA TOVUTI.

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu EAG Group Iman Kajula Wa Pili (kushoto) akipokea hati ya Kimila ya eneo walillonunua bagamoyo kwajili ya Jumuiya hiyo.
Jumuiya iliyoasisiwa na wakazi wa Kilima hewa Salasala jijini Dar es salaam likiwa na malengo ya kijamii na kiuchumi. Tangu kuasisisiwa SVG imetekeleza miradi Mingi kwenye eneo la Salasala ikiwemo kupanda miti zaidi ya 5,000, kutengeneza barabara, kutengeneza viwanja vya michezo na kulinda maeneo ya wazi, Ulinzi, kutengeneza gari la polisi na misaada ya miradi mbalimbali endelevu ikiwamo kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa Salasala
 
SVG haikuishia hapo, imeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya Wanachama wake. Mradi mkubwa uliotekelezwa ni pamoja na kununua hekari 250 huko Fukayosi Bagamoyo. Baada ya ununuzi huu mchakato wakupata hati ulifanywa na kufanikiwa kupata hati za kimila na kukabidhiwa kwa wanachama wa SVG ili kuanza kuendeleza maeneno hayo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Aridhi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Kibona aliipongeza SVG kwa kuwa kikundi kilicho makini na kutumia dhima ya umoja ni nguvu, alisema hati za kimila zina faida nyingi sana ikiwamo kutokuwa na kipindi cha ukomo ikilinganishwa na hati za kawaida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SVG Yahaya Banka alisema ‘’ SVG inalenga kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanachama wake na familia zao. Tunaamini kwa kutumia nguvu ya umoja tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika eneo letu tunaloishi pia kwa familia za wanachama’’

BTREAKING NEWZ DK MAGUFULI MGOMBEA WA URAIS CCM AWACHAKAZA MIGIRO NA AMINA

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 1560 akifuatiwa na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 702 huku Balozi Amina Salum Ali akipata kura 349.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Dk. Magufuli amepita kwa kura hizo kutokana na nguvu yake dhidi ya wagombea wengine.
“Hakukuwa na namna hapa kwa kuwa, wajumbe wanaamini katika mazingira haya magumu ya upinzani Dk. Magufuli anaaminika na kukubalika nje kuliko hawa wengine,” anasema mtoa taarifa na kuongeza;  

BONYEZA HAPA KUSOMA MATOKEO YOTE

WEMA SEPETU ALIINGIA MITINI KISA DIAMOND KATIKA SHEREHE HII YA SHOSTI AKE AUNTY EZEKEL

ZARI BOSS LADY AWEKA PICHA MATATA,MTOTO WAKE ANAUMWA

THE MAGAZETI YA BONGO LEO SUNDAY /JUMAPILI 12/7/2015 LIVE!!

MANENO 177 YA BUSARA SIKU YA LEO TOKA KWA JANUARY MAKAMBA.

$
0
0
Mchakato wa kumpata Mgombea wa Chama chetu umekamilika. Nampongeza kwa dhati Ndugu John Pombe Magufuli kwa kupata heshima ya kukiwakilisha Chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu kwa nafasi ya Urais. Naamini atarejesha imani ya wananchi kwa Chama chetu. Sina shaka atainadi vyema Ilani ya Chama chetu na kutupatia ushindi wa kishindo pamoja na kuunda Serikali itakayoakisi matarajio ya Watanzania walio wengi. Jukumu letu wana-CCM wote ni kumnadi kwa nguvu moja.
Nawashukuru wote kwa pongezi zenu za Tano Bora. Nawashukuru wale wote mlioonyesha imani yenu kwangu tangu mwanzo na wengine wote mliotuunga mkono. Mlitupa nguvu. Nawashukuru pia mliotupinga na kutukosoa. Mlitusaidia kujitazama na kujirekebisha.

UMOJA WA UKAWA WALINDWA NA MABAUNSA.

$
0
0
Jana Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza kuhusu makubaliano yao jijini Dar es Salaam  mgombea urais wa vyama hivyo,Wamekubaliana kumtangaza mgombea huyo tarehe kumi na nne jumanne ijayo.

RAIS KIKWETE AMSHUKURU ALLAH KWA MCHAKATO KWENDA SALAMA BILA MPASUKO.


DUKA JIPYA FELTRON SASA LIMEFUNGULIWA!

$
0
0





Fika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Opp. na DDC Kariakoo kwa ajili ya bidhaa za kisasa za majumbani na maofisini.

LAZARO NYARANDU ATETEWA NA MKE WAKE.

BREAKING NEWS WATU KADHAA WAUWAWA, SILAHA ZAPORWA BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI CHA SITAKISHARI, UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM USIKU HUU

ALI KIBA ASEMA DIAMOND AKIMTUMIA PICHA ZA TUZO NAZOWANIA MTV ATAZIPOST INSTAGRAM

$
0
0

Ali Kiba amefunguka hayo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM na B Dozen alipokuwa akifanya mahojiano maalum,alisema kuwa ana washangaa sana baadhi ya mashabiki wanasema kuwa hatoi sapoti kwa baadhi ya wasanii lakini yeye wakati anatoa kava za video yake ya Cheketua aliwatumia baadhi ya wasanii,ambao wapo walipost kwenye akaunti zao za Instagram lakini wengine hawakufanya hivyo lakini hajalalamika. 
‘’Kwanza niseme kuwa sina bifu na Diamond na hajanitumia picha nipost kwenye akaunti yangu ya Instagram kama angenitumia ningepost kwani sina tatizo naye,’alisema Ali Kiba.  

BREAKING NEWS WATU KADHAA WAUWAWA, SILAHA ZAPORWA BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI CHA SITAKISHARI, UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>