Stay Tuned: Tunatarajia kutengeneza njia mahali hapa ambapo panaonekana hakuna njia. Siyo sahihi kuwaachia nchi na hatima ya nchi watu ambao hawakutoa hata tone moja la jasho kupigania mabadiliko ya siasa.

Iweje leo hii baada ya yote ambayo watu wamesimamia wengine kwa damu na wengine hata kwa uhai wao waje watu wavune wasichopanda kwa ahadi kuwa ati na sisi tutakula nao watakachovuna?

Kesho Inshallah, tutaweka hoja zetu wazi ili wao waamue kama wanataka kuungwa mkono nasi au la; hatutaki wao watuwekee masharti ya sisi kuwaunga wao mkono au kutupigisha mikwara ya kwanini tukae kimya ili wao wafanye wanalotaka.

Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho!

MM

NB: Nitajaribu kutoa majibu ya hoja zilizotolewa na baadhi ya watu (ikiwemo ile mada ya Character X) kuhusiana na kuunga mkono hili la Lowassa.