Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MKUU CHUO CHA GTI, BI. ZUKI MIHYO AFUNGUA MAFUNZO YA JINSIA, DEMOKRASIA NA KATIBA

$
0
0

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya.

MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo leo jijini Dar es Salaam amefungua mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yaliyowashirikishwa washiriki kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani na Morogoro.
Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi. Zuki Mihyo alisema kutokuwepo na misingi imara ya kutetea, kulinda na kudumisha demokrasia iliyojengwa kwenye misingi ya usawa wa kijinsia inayo tambulika Kikatiba kumechangia uwepo wa tatizo la unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Alisema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia licha ya kuwapata watu wa jinsia zote, limekuwa likiwaathiri zaidi wanawake na watoto wa kike tofauti na ilivyo kwa wanaume na watoto wa kiume katika jamii, hivyo kushauri kuna kila sababu ya kupambana na mifumo kandamizi inayochangia hali hiyo.
“…Wanawake na watoto wa kike mara nyingi wamekuwa wakifanyiwa ukatili huu na wanaume au wavulana ambao wanaweza kuwa ndugu zao wa karibu, marafiki na hata wenzi wao,” alisema Mkuu huyo wa chuo cha GTI kilichopo chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo.
Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo.
Alisema suala la ukekelezaji wa mila na desturi kama vile ukeketaji, kurithi wajane na mila nyingine nyingi zinazowagandamiza wanawake na makundi ya pembezoni na kuwafanya kutokuwa na sauti wala kushiriki katika kutoa uamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa vimekuwa vikichangia ukatili wa jinsia kwa wasichana, wanawake na makundi mengine ya pembezoni.
“…Tunaelewa kuwa wakati wa zamani mila nyingi zilikuwa na maana lakini kwa wakati huu mila hizo zimepitwa na wakati hivyo ziachwe ili kukomesha dhuluma, manyanyaso, ukandamizaji n.k, ili kuwa na usawa kwa watu wote,” alisema.
Aidha alifafanua kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa washiriki kuweza kushiriki katika kuchambua masuala ya jinsia, demokrasia na katiba mpya ili waweze kuyasimamia na kuyatetea katika mikakati mbalimbali ya maendeleo. Aliongeza kuwa malengo mahususi ni pamoja na kukuza uelewa na utambuzi wa uhusiano baina ya dhana za jinsia, demokrasia na katiba, kuchochea ushiriki na uwajibikaji wa asasi za kiraia na makundi maalumu yaliopo pembezoni na mchakato wa kidemokrasia na kutambua changamoto na fursa zilozopo katika kuingiza masuala ya jinsia na demekrasia kwenye katiba mpya.
Akifafanua zaidi juu ya mafunzo hayo, mmoja wa watoa mada, Geoffrey Chambua alisema washiriki wanatoka katika ngazi ya jamii; yaani katika asasi za kiraia, vikundi vya kijamii, asasi za kidini, wajasiliamali na makundi maalumu wote kutoka katika mikoa ya Morogoro, Lindi, Pwani pamoja na Dar es Salaam yenyewe. Chambua alisema mafunzo kama hayo pia yanaendelea katika kanda anuai.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles